Athumani Idd Chuji Kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga, amesema
kuwa uwezo wake kamwe hauwezi kuulinganisha na Mbrazili Emerson Roque ambae ni
kiungo mpya wa timu hiyo.
Emerson tayari yuko jijini
Dar es Salaam ambapo tayari ameanza mazoezi na timu ya Yanga.
Chuji alitupiwa viragoooo na
Yanga katika usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara baada ya mkataba wake
kumalizika kabla ya kwenda Oman kwenye majaribio na kurejea nchini kwa kile
kilichoelezwa kushindwa, akiwa na Betram Mwombeki na Mkenya, Jerry Santo.
Hata hivyo Chuji kwa sasa
yupo katika timu ya Mwadui FC ya shinyanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza
ambapo ameweka wazi kuwa yeye ni jembe kuliko Emerson.