KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah amemteua rafiki yake wa siku nyingi Prince Owusu kuwa msaidizi wake katika kibarua chake kipya huko nchini Sudan.
Mara baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Al-Khartoum Appiah aliamua kumvuta Owusu kuwa msaidizi wake baada ya wawili hao kufanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu sasa.

Wawili hao wanatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Sudan Desemba 10 mwaka huu tayari kuanza kazi yao hiyo mpya.
Al-Khartoum iko katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo na wanatarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani.