Saturday, May 25, 2013

30 TWIGA STARS WAITWA KAMBINI KESHO MEI 26 MWAKA HUU

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.

Twiga Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu) ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi kwenye klabu zao.

Kambi hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.

Wachezaji walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).

Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).

Nabila Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

RCL KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO
Raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26 mwaka huu) kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.


Abajalo ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Nayo Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Leo (Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, May 24, 2013

UCL: WATOTO WA BABA MMOJA USO KWA USO WEMBLEY

NI FAINALI ya kukata na shoka  hapo Kesho katika dimba la  uwanja wa wembley uliopo jijini london nchini uingereza watoto wa baba mmoja kutoka ujerumani watavaana  kucheza Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya  ambapo Borussia Dortmund na Bayern Munich watakukutana hapo  kesho Jumamosi Mei 25 na kila upande imejipanga kuhakikisha inaibuka na ushindi hasa kisaikolojia
Hii ni mara ya kwanza kwa Klabu za Germany kukutana Fainali ya UCL, hii itakuwa mara ya 4 kwa Klabu za Nchi moja kukutana Fainali hizi.
Mwaka 2000, Klabu za Spain, Real Madrid na Valencia, zilivaana, Mwaka 2003 AC Milan na Juventus za Italy zilipigana na 2008 ni Man United v Chelsea za England.
Kwa Bayern Munich hii ni Fainali yao ya 10 ya Klabu Bingwa Ulaya wakiwa nyuma ya Real Madrid, waliofika Fainali 12, na AC Milan, Fainali 11,
Hii itakuwa Fainali ya 3 kwa Bayern ndani ya Misimu minne iliyopita lakini mara ya mwisho kutwaa Kombe la UCL ni Mwaka 2001.
Kwa Borussia Dortmund, hii ni Fainali ya Pili kwao ambapo walishinda ile ya kwanza ya Mwaka 1997.
Baada ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka 1997, Msimu uliofuata, 1997/98, Borussia Dortmund na Bayern Munich zilikutana Robo Fainali ya UCL na Borussia kusonga kwa Jumla ya Bao 1-0.

KLABU ZA NCHI MOJA KUUMANA FAINALI ULAYA

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
1999/2000 Real Madrid 3-0 Valencia CF
2002/03 AC Milan 0-0 Juventus (AC Milan washinda kwa Penati 3-2)
2007/08 Manchester United 1-1 Chelsea FC (Man United washinda kwa Penati 6-5)
UEFA CUP
1979/80 VfL Borussia Mönchengladbach 3-2 Eintracht Frankfurt

WAPI WAMETOKA MPAKA KUFIKA FAINALI:
FAHAMU:  -N: Nyumbani -U: Ugenini
BORUSSIA DORTMUND BAYERN MUNICH
KUNDI  D: KUNDI  F:
MSHINDI MSHINDI
-Ajax: 1-0 [N] 4-1 [U] -Valencia: 2-1 [N] 1-1 [U]
-Man City: 1-1 [U]] 1-0 [N] -BATE Borislov:1-3 [U] 4-1 [N]
-Real Madrid: 2-1 [N] 2-2 [U] Lille: 1-0 [U] 6-1 [N]
RAUNDI ZA MTOANO: RAUNDI ZA MTOANO:
-Donetsk: 2-2 [U] 3-0 [N] -Arsenal: 3-1 [U] 0-2 [N]
-Malaga: 0-0 [U] 3-2 [N] -Juventus: 2-0 [N] 2-0 [U]
-Real Madrid: 4-1 [N] 2-0 [U] -Barcelona: 4-0 [N] 3-0 [U]

DONDOO MUHIMU:
REFA:
-Nicola Rizzoli [Italy] akisaidiwa na wenzake toka Italy Renato Faverani na Andrea Stefani na Refa wa Akiba, Damir Skomina, wa Slovenia.
BALOZI MAALUM:
-Steve McManaman, Mshindi mara mbili wa UCL, ni Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa England
SHERIA ZA FAINALI:
-Baada Dakika 90 kama Sare, zitachezwa Dakika za Nyongeza 30 na kama bado Sare ni Mikwaju ya Penati kuamua Bingwa.
-Kila Timu itakuwa na Wachezaji wa Akiba 7
-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji Watatu tu.
UWANJA: Wembley Stadium
-Ndio Uwanja wa Nyumbani wa Timu ya Taifa ya England.
-Ingawa ndio ilichezwa Fainali ya UCL Mwaka 2011, UEFA imeuteua tena kwa kuadhimisha Miaka 150 ya uhai wa FA, Chama cha Soka England.
-Ni mara ya 7 kwa Wembley kutumika kwa Fainali za Klabu Bingwa Ulaya nyingine zikiwa za Miaka ya 1963, 1968, 1971, 1978, 1992 na 2011.
-Katika Fainali za Miaka ya 1968 na 1978, Klabu za England zilitwaa Ubingwa kwa Mwaka 1968 Manchester United kuichapa Benfica Bao 4-1 na Liverpool kuifunga Club Brugge 1-0 Mwaka 1978.
MATOKEO MICHIZO ZA HIVI KARIBUNI
[BUNDESLIGA PAMOJA NA DFB POKAL]
04/05/13      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 1
27/02/13      Bayern Munich v Borussia Dortmund       1 : 0
01/12/12      Bayern Munich v Borussia Dortmund       1 : 1
12/08/12      Bayern Munich v Borussia Dortmund       2 : 1
12/05/12      Borussia Dortmund v Bayern Munich       5 : 2
11/04/12      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 0
19/11/11      Bayern Munich v Borussia Dortmund       0 : 1
26/02/11      Bayern Munich v Borussia Dortmund       1 : 3
03/10/10      Borussia Dortmund v Bayern Munich       2 : 0
13/02/10      Bayern Munich v Borussia Dortmund       3 : 1
12/09/09      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 5
08/02/09      Bayern Munich v Borussia Dortmund       3 : 1
23/08/08      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 1
23/07/08      Borussia Dortmund v Bayern Munich       2 : 1
19/04/08      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 2
13/04/08      Bayern Munich v Borussia Dortmund       5 : 0
28/10/07      Borussia Dortmund v Bayern Munich       0 : 0
26/01/07      Borussia Dortmund v Bayern Munich       3 : 2
11/08/06      Bayern Munich v Borussia Dortmund       2 : 0
13/05/06      Bayern Munich v Borussia Dortmund       3 : 3
17/12/05      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 2
19/02/0        Bayern Munich v Borussia Dortmund       5 : 0
18/09/04      Borussia Dortmund v Bayern Munich       2 : 2
17/04/04      Borussia Dortmund v Bayern Munich       2 : 0
09/11/03      Bayern Munich v Borussia Dortmund       4 : 1
19/04/03      Borussia Dortmund v Bayern Munich       1 : 0
Ukitazama kuelekea mchezo wa kesho Bayen munich inanafasi kubwa kutwaa kombe hili lakini ukitazama zaidi timu hizi zinaupinzani wa hali ya juu hivyo timu ambayo itakuwa imejipanga na kufanya maandalizi mazuri basi inanafasi ya kutwaa ubingwa msimu wa UCL UEFA CHAMPION LIGI MSIMU WA 2012-2013

 TAZAMA MSIMO WA BUNDASLIGA
*FAHAMU NI BINGWA BAYERN MUNICH BUNDASLIGA
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Bayern Munich
34
28
4
1
94
18
82
92
2
BV Borussia Dortmund
34
19
9
5
80
42
41
66










MABINGWA WALIOPITA WA UCL

MWAKA               BINGWA


1955–56 Real Madrid
1956–57 Real Madrid
1957–58 Real Madrid
1958–59 Real Madrid
1959–60 Real Madrid
1960–61 Benfica
1961–62 Benfica
1962–63 Milan
1963–64 Internazionale
1964–65 Internazionale
1965–66 Real Madrid
1966–67 Celtic
1967–68 Manchester United
1968–69 Milan
1969–70 Feyenoord
1970–71 Ajax
1971–72 Ajax
1972–73 Ajax
1973–74 Bayern Munich
1974–75 Bayern Munich
1975–76 Bayern Munich
1976–77 Liverpool
1977–78 Liverpool
1978–79 Nottingham Forest
1979–80 Nottingham Forest
1980–81 Liverpool
1981–82 Aston Villa
1982–83 Hamburg
1983–84 Liverpool
1984–85 Juventus
1985–86 Steaua BucureČ™ti
1986–87 Porto
1987–88 PSV Eindhoven
1988–89 Milan
1989–90 Milan
1990–91 Red Star Belgrade
1991–92 Barcelona
1992–93 Marseille
1993–94 Milan
1994–95 Ajax
1995–96 Juventus
1996–97 Borussia Dortmund
1997–98 Real Madrid
1998–99 Manchester United
1999–2000 Real Madrid
2000–01 Bayern Munich
2001–02 Real Madrid
2002–03 Milan
2003–04 Porto
2004–05 Liverpool
2005–06 Barcelona
2006–07 Milan
2007–08 Manchester United
2008–09 Barcelona
2009–10 Internazionale
2010–11 Barcelona
2011–12 Chelsea




















WENYEVITI WA FA NDIYO WASIMAMIZI RCL WIKIENDI HII

WAKATI Mechi za kwanza za raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zinachezwa wikiendi hii, Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesisitiza kuwa wasimamizi wa mechi za ligi hiyo ni wenyeviti wa mikoa wa vyama vya mpira wa miguu.

Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Ramadhan Nassib ilikutana jana (Mei 23 mwaka huu) kupitia ripoti za makamishna kwa mechi za raundi ya kwanza ya RCL iliyomalizika wikiendi ya Mei 18 na 19 mwaka huu.

Kuhusu viwanja vinavyotumika kwa ligi hiyo, Kamati imesema vitaendelea kuwa vile vya makao makuu ya mikoa, na kwa vile vilivyokuwa vimeombwa vifanyiwe marekebisho ili viweze kukaguliwa kwa ajili ya RCL msimu ujao. Pia imeitaka mikoa kuendelea kuboresha viwanja vinavyotumika sasa, lakini vina upungufu.

Vilevile Kamati imebaini kuwa zimekuwepo pingamizi kuhusu usajili wa wachezaji ambapo imesema haiwezi kujadili pingamizi hizo kwa vile mikoa yote haikuwasilisha usajili wa wachezaji wa klabu husika uliofanyika mikoani kama ilivyoagizwa na kuelekezwa na TFF.

Hata hivyo, Kamati imeitaka mikoa ambayo klabu zao zimefanikiwa kuingia raundi ya pili kuwasilisha usajili huo haraka.

Pia Kamati imebaini kuwa zipo baadhi ya klabu ambazo zimekata rufani kuhusu usajili wa baadhi ya wachezaji, na kusisitiza kilichowasilishwa ni pingamizi kwa vile kwa mujibu wa kanuni masuala ya uwanjani hayakatiwi rufani. Hivyo, Kamati imeshauri klabu zilizokata rufani zilirejeshewe ada zilizolipa kwa ajili hiyo.

Makamishna na waamuzi wanaosimamia mechi za RCL wamekumbushwa kuwa ili mchezaji aruhusiwe kucheza mechi ni lazima awe na leseni yake (kadi ya usajili), vinginevyo asiruhusiwe kucheza mechi husika.
Mechi za RCL zinaendelea wikiendi hii ambapo zote zitachezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) isipokuwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi.

Nayo mechi kati ya Abajalo ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi iliyokuwa ichezwe Jumamosi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam sasa itachezwa Jumapili kwa vile siku hiyo uwanja huo utatumika kwa mazoezi ya Taifa Stars.

Mechi nyingine za RCL zitakazochezwa Mei 26 mwaka huu ni Machava FC ya Kilimanjaro dhidi ya Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi.

Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

SEMINA YA USAJILI- TMS KUFANYIKA MEI 25
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya usajili kwa njia ya mtandao (Transfer Matching System-TMS) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2013/2014.

Semina hiyo itafanyika Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF saa 3 kamili asubuhi ikishirikisha watu wawili kutoka kila klabu ambao ni TMS Manager, na ofisa mwingine wa klabu.

Klabu za ligi hiyo zinazotakiwa kuhudhuria semina ya usajili ni Ashanti United, Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Oljoro JKT, Rhino Rangers, Ruvu Shooting, Simba, Tanzania Prisons na Yanga.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, May 23, 2013

CITY YAKANUSHA KUWAWINDA FALCAO NA NEYMAR

NEYMAR_THE_BRAZILIAN
MKURUGENZI MKUU wa Manchester City chief Ferran Soriano amekanusha taarifa kuwa wanahaha kuwasaini Masupastaa Radamel Falcao na Neymar.
Hivi karibuni kumezagaa ripoti kuwa Man City ni miongoni mwa Klabu zinazokimbiza saini za Straika wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, na yule wa Santos ya Brazil, Neymar.
Falcao anawindwa na msululu wa Klabu zikiwemo Chelsea, Monaco na Real Madrid baada ya kung’ara sana kwa kuifungia Atletico Mabao muhimu kwa Misimu kadhaa.
Nae Neymar, anaewindwa na Klabu kubwa Barani Ulaya, anatarajiwa kuihama Brazil baada ya Nchi hiyo kuwa Mwenyeji wa Kombe la Dunia Mwaka 2014.
Hata hivyo, Soriano amekanusha kwa kutamka: “Neymar na Falcao? Habari hizo ni uongo, hawajawahi kuwa kwenye ajenda yetu!”
Vile vile, Soriano aliponda habari kuwa wanataka kumuuza Straika wao mahiri Serio Aguero, mwenye Miaka 24, huku Real Madrid ikitajwa kuwa ndio atatua.
Soriano amesisitiza: “Hatujawahi kufikiria kumuuza Aguero. El Kun ana furaha kubaki kwetu Mwaka huu!”

MESSI AFURAHIA KUVAA JEZI NAMBA 10 AKIWA KATIKA TIMU HIYO.

MSHAMBULIAJI nyota maarufu dunia wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amesema anajisikia raha na heshima kubwa kuvaa jezi namba 10 akiwa katika klabu hiyo na kufuata nyayo za Ronaldinho na nyota wengine waliokuwa wakivaa jezi hiyo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alirithi namba ya jezi ya Ronaldinho wakati nyota huyo wa Brazil alipoondoka Barcelona kwenda AC Milan katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2008 na kudai kuwa ilikuwa na maana kubwa kwake wakati anaanza kuivaa. Messi amesema wakati anapewa jezi hiyo namba 10 alijisikia furaha kwa ni jezi ambayo imekuwa ikivaliwa na wachezaji waliofanya mambo makubwa katika klabu hiyo. Nyota huyo pia alielezea nia yake ya kutaka kuiongoza timu ya taifa ya nchi yake kunyakuwa Kombe la Dunia huku akitaka mataji zaidi katika klabu yake ya Barcelona.

MOURINHO PAMOJA NA RONALDO WAFUNGIWA MECHI 2.

Kocha wa Real madrid Jose Mourinho pamoja na nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo wamefungiwa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa nje katika fainali dhidi ya Atletico Madrid. Mourinho mwenye umri wa miaka 50 alitolewa nje baada ya kumshambulia mwamuzi kwa maamuzi aliyotoa adhabu ambayo hataweza kuitumikia baada ya kutangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu. Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 alipewa kadi nyekundu baada kukutwa na hatia ya kumpiga teke la uso kwa makusudi mchezaji wa Atletico, Gabi. Wote wawili Ronaldo na Mourinho watakuwepo katika michezo miwili ya mwisho ya ligi ya Madrid.

TIMU YA TAIFA YA CAMEROON YAPATA KOCHA MPYA.

Timu ya taifa ya Cameroon imefanikiwa kupata kocha mpya  Volker Finke kuwa kocha mkuu wa timu hiyo huku kibarua chake cha kwanza Mjerumani huyo ni kuhakikisha timu hiyo inafuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Finke anachukua nafasi ya kocha wa muda wa timu hiyo Jean-Paul Akono ambaye aliwekwa hapo kuziba nafasi ya Denis Lavagne Septemba mwaka jana baada ya Mfaransa huyo kushindwa kuisaidia timu hiyo kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2012 na 2013. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 aliwahi kuifundisha klabu ya SC Freiburg kuanzia mwak 1991 mpaka 2007 na atakuwa anafundisha kikosi cha timu ya taifa kwa mara ya kwanza baada ya kutemwa na timu ya Urawa Red Diamonds ya Japan na timu ya Cologne ya nchini kwake. Katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, Cameroon wako kileleni mwa kundi I wakiwa na alama sita katika mechi tatu walizocheza wakifuatiwa na Libya wenye alama tano, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC alama nne na Togo alama moja. Kazi yake ya kwanza Finke itakuwa ni kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ukraine utakaochezwa jijini Kiev Juni 2 mwaka huu kabla ya kuhamishia nguvu zao katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Togo Juni 9, DRC Juni 16 na Libya Septemba 6 mwaka huu