Wednesday, February 12, 2014

REAL MADRID KUISUBIRI MSHINDI KATI YA REAL SOCIEDAD v BARCELONA LEO:

Nyota Mahiri Duniani Cristiano Ronaldo Jana Usiku Aliiwezesha Real Madrid kutingaFainali ya Copa del Rey baada ya kuibwaga Atletico Madrid  kwenye Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali iliyochezwa Estadio Vicente Calderon.
Penati hizo za Ronaldo zilipatikana katika Dakika ya 7 na 16 na kuwabwaga nje Atletico Madrid ambao ndio walikuwa Mabingwa Wateteza wa Kombe hili.
hivyo basi Real wametinga Fainali kwa Jumla ya Bao 5-0 baada kushinda Mechi ya Kwanza 3-0 huko Santiago Bernabeu Wiki iliyopita.
Kwenye Fainali Real itacheza na Mshindi wa Leo kati ya Real Sociedad na Barcelona ambao wanarudiana huko Estadio Anoeta huku Barcelona wako mbele kwa Bao 2-0 walizopata huko Nou Camp Wiki iliyopita.
COPA_DEL_REY-FP
COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 2 [0-5] [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [0-2] [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19
Real Madrid v Real Sociedad/Barcelona

KAZI IPO LEO ARSENAL VS MAN UNITED-UWANJANI EMIRATES

Jumatano Februari 12

2245 Arsenal v Man United

2245 Everton v Crystal Palace

2245 Man City v Sunderland

2245 Newcastle v Tottenham

2245 Stoke v Swansea

2300 Fulham v Liverpool

MSIMAMO:

NA TIMU P W D L F A PTS GD
1 Chelsea FC 26 17 6 3 48 21 27 57
2 Arsenal FC 25 17 4 4 48 26 22 55
3 Man City 25 17 3 5 68 27 41 54
4 Liverpool 25 15 5 5 63 30 33 50
5 Tottenham 25 14 5 6 32 32 0 47
6 Everton FC 25 12 9 4 37 26 11 45
7 Man United 25 12 5 8 41 31 10 41
8 Southampton 26 10 9 7 37 29 8 39
9 Newcastle 25 11 4 10 32 34 -2 37
10 Swansea 25 7 6 12 32 35 -3 27
11 Hull City 26 7 6 13 25 31 -6 27
12 West Ham 26 7 7 12 28 33 -5 28
13 Aston Villa 26 7 7 12 27 36 -9 28
14 Stoke City 25 6 8 11 26 40 -14 26
15 Crystal Palace 25 8 2 15 18 34 -16 26
16 Norwich City 26 6 7 13 19 39 -20 25
17 West Brom 26 4 12 10 30 38 -8 24
18 Sunderland 25 6 6 13 25 38 -13 24
19 Cardiff City 26 5 7 14 19 44 -25 22
20 Fulham FC 25 6 2 17 24 55 -31 20

RATIBA MECHI ZIJAZO:

Jumamosi Februari 22

1545 Chelsea v Everton

1800 Arsenal v Sunderland

1800 Cardiff v Hull

1800 Man City v Stoke

1800 West Brom v Fulham

1800 West Ham v Southampton

2030 Crystal Palace v Man United

Jumapili Februari 23

1630 Liverpool v Swansea

1630 Newcastle v Aston Villa

1900 Norwich v Tottenham

RIPOTI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA WAKAZI WA PWANI UKANDA WA PWANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI:


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI 
         MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700
Barua pepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: Tanzania Meteorological Agency - Admin -

S.L.P. 3056
DAR ES SALAAM
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622

10 Februari, 2014

Taarifa kwa Umma: Matarajio ya kuwa naVipindi vya Mvua kubwa, Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa.
Taarifa Na.
201402-01
Muda wa Kutolewa: Saa za Afrika Mashariki
Saa 11 Jioni
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia: Tarehe
11 Februari, 2014
Mpaka: Tarehe
13 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
1. Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24)
2. Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa
pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0
Kiwango cha uhakika:
Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa
kuathirika
1. Vipindi vya Mvua Kubwa: Ukanda wa pwani mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya
Unguja na Pemba, Mbeya , Njombe, Ruvuma pamoja na kusini
mwa mkoa wa Morogoro
2. Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa: Pwani ya mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FOBANE” kusini
magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu.
Angalizo:
Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo pale itakapobidi

WAZIRI UMMY MWALIMU AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA MADIWANI WANAWAKE KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA TANGA

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS,UMMY MWALIMU AKIUZNGUMZA WAKATI WA WARSHA YA MAFUNZO KWA MADIWANI WOTE WANAWAKE KUTOKA HALMASHAURI ZOTE MKOANI TANGA.
BAADHI WA WASHEMIWA MADIWANI KUTOKA HALMASHAURI MBALIMBALI MKOANI TANGA WAKIFUATILIA MADA MBALIMBALI KWENYE WARSHA YA MAFUNZO KWA MADIWANI WANAWAKE .










MJUMBE WA BODI YA  TAWODE NA MWENYEKITI WA JUMUIYA WA UMOJA WA VIJANA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA TANGA (UVCCM),ABDI MAKANGE AKIZUNGUMZA KWENYE MAFUNZO HAYO LEO
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO KULIA AKIWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TAWODE FATUMA MGANGA KUSHOTO KWENYE MAFUNZO HAYO LEO
NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS UMMY MWALIMU KATIKATI KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO NA KULIA NI KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA WAKIWA KWENYE WARSHA YA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA MADIWANI WOTE MKOA WA TANGA.  
HAPA WAKIPIGA MAKOFI.
NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS UMMY MWALIMU KATIKATI KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO  NA KULIA NI KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA LEO WAKATI WA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA MADIWANI WANAWAKE KUTOKA HALMASHAURI ZOTE ZA JIJI LA TANGA

Sunday, February 9, 2014

SERIE A: JUVE YALAZIMISHWA SARE YA BAO 2-2 VS VERONA-TEVEZ ATUPIA

MBALI ya Juventus kutangulia kwa Bao 2 za mapema kupitia Carlos Tevez, Hellas Verona walijipanga na hatimaye kurudisha Bao zote na kupata Sare ya Bao 2-2 walipocheza na Mabingwa hao wa Italy ambao pia ni Vinara wa Serie A huko Italy.

Baada Tevez kupiga Bao 2, Luca Toni aliifungia Hellas Verona Bao la kwanza na Muargetina Juanito Gomez kusawazisha katika Dakika ya 94.

Baada ya hii Leo Timu ya Pili AS Roma nao kubanwa na kutoka Sare 0-0 Lazio, Juve wamebaki kileleni wakiwa Pointi 9 mbele ya AS Roma na wako Pointi 13 mbele ya Timu ya Tatu Napoli ambao waliifunga AC Milan 3-1 hapo Jana Jumamosi.

RATIBA/MATOKEO:

Jumapili Februari 9

Torino 1 Bologna 2

Lazio 0 AS Roma 0

Parma 0 Catana 0

Sampdoria 1 Cagliari 0

Livorno 0 Genoa 1

Hellas Verona 2 Juventus 2

2245 Inter Milan v Calcioa

MSIMAMO-Timu za Juu:

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Juventus FC 23 19 3 1 56 18 38 60
2 AS Roma 22 15 6 1 45 11 34 51
3 SSC Napoli 23 14 5 4 47 27 20 47
4 Fiorentina 23 13 5 5 42 24 18 44
5 Hellas Verona 23 11 3 9 39 37 2 36
6 Inter Milan 22 8 9 5 39 27 12 33

TFF YATANGAZA BODI YA WADHAMINI NA KAMATI ZAKE!!

BOARD OF TRUSTEE; Said Hamad El-Maamry, Stephen Mashishanga, Dr Ramadhan Dau, Joel Bendera, Mohamed Abdul Aziz

Kamati ya Nidhamu; Tarimba Abbas (Mwenyekiti), Advocate Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma, Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu; Profesa Mgongo Fimbo (Mwenyekiti), Advocate Hamidu Mbwezeleni (Makamu Mwenyekiti), Titus Bandawe, Twaha Mtengera, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Kamati ya Maadili; William Erio (Mwenyekiti), Advocate Ezekiel Maganja (Makamu Mwenyekiti), Advocate Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili; Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
Kamati ya Uchaguzi; Advocate Melchesedeck Lutema (Mwenyekiti), Advocate Walter Chipeta (Makamu Mwenyekiti), Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura, Hassan Dalali.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi; Advocate Julius Lugaziya (Mwenyekiti), Advocate Mwita Waissaka (Makamu Mwenyekiti), Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga, Masoud Issangu.
Kamati ya Fedha na Mipango; Wallace Karia (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammad, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy, Cyprian Kuhyava.
Kamati ya Mashindano; Geofrey Nyange (Mwenyekiti), Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald Ambi, Davis Mosha, Said George, Nassoro Idrissa (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Ufundi; Kidao Wilfred (Mwenyekiti), Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedastus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo, Dk. Cyprian Maro (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana; Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti), Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya, Ibrahim Masoud (Mshauri wa Ufundi wa Rais- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake; Lina Kessy (Mwenyekiti), Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amina Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o, Ingridy Kimaro.
Kamati ya Waamuzi; Saloum Umande Chama (Mwenyekiti), Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi, Zahra Mohamed.
Kamati ya Habari na Masoko; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela, Juma Pinto.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji; Advocate Richard Sinamtwa (Mwenyekiti), Advocate Moses Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hans Poppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko, Imani Madega.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha; Ramadhan Nassib (Mwenyekiti), Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga, Elias Mwanjala.
Kamati ya Tiba; Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema, Asha Sadick.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni; Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti), Shaffih Kajuna Dauda (Makamu Mwenyekiti), Boniface Pawasa, Deo Lucas, Juma Mgunda, John Kanakamfumu, John Mwansasu.
AD HOC COMMITTEES
Kamati ya Kutathimini Muundo wa Ligi; Dk. Mshindo Msolla (Mwenyekiti),Idd Mshangama (Katibu), Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir, Lucas Kisasa.
Kamati ya Kutathimini Muundo wa Bodi ya Ligi; David Nchimbi (Mwenyekiti), Edwin Kidifu, Jones Paul, Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani, Pelegrinius Rutayuga.

SIMBA YABAMIZWA NA WAZEE WA KWATA JKT MGAMBO

WEKUNDU wa Msimbazi Simba imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kwa mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa adhabu. Wachezaji wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.
Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.