Mshambuliaji Mahiri wa Galatasaray ya Uturuki,
akiwa na wenzake amefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa
na Chelsea.
Mara tu baada ya mazoezi, Drogba amesema
yuko tayari kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya kikosi hicho cha Jose Mourinho
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Nimerudi tena hapa, kwangu ni sehemu
bora na yenye kumbukumbu nyingi sana. Lakini kama ni mechi, niko tayari,"
alisema Drogba.
Katika mechi ya kwanza jijini Istambul,
timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Hivyo jibu litatapikana leo.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]