Wednesday, September 10, 2014

JE TUFIKA KUHUSU TAIFA STARS HII AMA NDIO MWISHO

Hakuna kitu kinawaumiza watanzania kuhusu kilio kikubwa cha wadau na wapenzi wa soka nchini Tanzania ni kuitaka serikali, TFF na vyama wanachama wake pamoja na klabu zote kuwekeza katika soka la vijana kwa manufaa ya Taifa.
Tatizo la soka la Tanzania ni la kimfumo. Hakujawa na njia sahihi ya kupata wachezaji na kusababisha kuborongo kwa muda mrefu.
Aina ya wachezaji wanaopatikana Tanzania ni wale wasiokuwa na misingi ya mpira tangu utotoni, kwasababu hakuna akademi za kisasa na hata za kawaida kwa maeneo mengi ya nchi hii, hivyo vijana wenye vipaji vya soka hujikuta hawana kwa kujiendeleza.
Soka la vijana ni muhimu na lazima Taifa kama Taifa liandae mpango mkakati wa kitaifa kwa malengo ya kuwa na falsafa ya Taifa na mfumo sahihi wa kuibua, kukuza na kulinda vipaji vya soka.
Marsh aliachishwa kazi ya kuinoa Stars sambamba na kocha Mdenish, Kim Poulsen kwa madai ya wawili hao kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa na Shirikisho la soka la Tanzania, TFF.
Hata hivyo wakati Kim anavunjiwa mkataba, Mashi alikuwa wodini akipata matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Usidhani huwa anakaa bure. Marsh ni moja ya watu wachache nchini wenye kiu ya kuona soka la nchi hii linapiga hatua.
Tangu mwaka 1991 anamiliki kituo chake cha kuibua, kulea na kukuza vipaji mkoani mwanza.

WADHAMINI WA VPL WAGAWA JEZI KWA TIMU ZA VPL KWA AJILI YA SEPT 20 VPL

Ikiwa zimebaki siku 10 kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2014-2015 wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom watoa jezi kwa vilabu vyote 14 vitakavyoshiriki ligi hiyo.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu za Ligi Kuu msimu mpya leo, Vodacom wamekabidhi jezi za rangi ya kijani na njano kwa Yanga na nyekundu na nyeupe kwa Simba, lakini muundo ni mmoja kila kitu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alihakikisha timu zote 14 za Ligi Kuu zinapatiwa vifaa hivyo.
Timu zote 14 zilituma wawakilishi wao katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam.  
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi, Azam FC wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo, wakati washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20.
Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumapili wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC.

MAJIMAJI YAWEKA HADHARANI KIKOSI CHAKE KWA AJILI YA LIGI DARAJA LA KWANZA

 ya zamani Tanzania, Majimaji FC WANALIZOMBE ya Songea mkoani Ruvuma imetaja kikosi cha wachezaji 26 iliyowasajili kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.
Ofisa Habari wa Majimaji ya Songea, Nathan Mtega ametaja kikosi cha msimu ujaoAmesema katika kikosi hicho, wachezaji 12 ni wapya ambao ni Oswald Issa, Samir Said, Emmanuel Maganga, Ally Mohamed, Kudra Omary, Said Fundikira, Mrisho Said, Idd Kipagule, Mohamed Omary, Yohana Kimburu na Msafiri Abdallah.
Amewataja wachezaji wa zamani 14 watakaoendelea kuitumikia klabu hiyo kuwa ni pamoja na Anthony Mwingira, Eliuta Ndunguru, Bahati Yussuf, Gerarrd Mbena, Abdallah Aus, Ditram Nchimbi, Filoteus Mahundi, Mpoki Mwakinyuke, Alex Zegega, Sadiq Gawaza, Odo Nombo, Frank Sekule, Marcel Boniventure na Freddy Mbuna.


Tuesday, September 9, 2014

STAND UNITED YAPATA UDHAMINI WA MWAKA MMOJA

klabu ya Stand United imeingia mkataba na Beki ya Exim Tanzania udhamini wa mwaka mmoja na inayojiandaa kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.
Stand United yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga itaanza kampeniza zake nyumbani kwa kuvaana na wageni wenzao wa ligi kuu, Ndanda fc kutoka Mtwara.
Taarifa zanaeleza kuwa katika mkataba hao, Stand United watalamba milioni 10 za Kitanzania.
Huu ni udhamini wa pili kwa klabu hiyo kwani tayari walishalamba udhamini wa kampuni ya Binslum sambamba na klabu za Mbeya City na Ndanda fc ya Mtwara.
Kwa maana hiyo, Stand United watakuwa wanakusanya fedha za udhamini kutoka Binslum, Azam TV na Benk ya Exim Tanzania.
Hivi karibuni wachezaji wa Stande United waliripotiwa kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara, lakini uongozi ukafafanua kuwa kuna mahali kulitokea tatizo na fedha zipo.
Viongozi hao walikiri kufanya uzembe na walifanikiwa kumaliza tatizo.
Kwa udhamini huu, Stand United watakuwa na uwezo wa kufanya mambo ya msingi klabu kwao.

PATA UFAFANUZI WA YANGA NA EMMANUELI OKWI HUU HAPA

UTANGULIZI
Kwa niaba ya mteja wetu, Emmanuel Arnold Okwi, napenda kutoa maelezo kuhusu Uamuzi wa kihistoria katika soka la Tanzania ambao umefanywa na Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF. Uamuzi huo ni wa kihistoria kwa misingi ifuatayo:

MOSI: Ni mara ya Kwanza katika historia ya soka la Tanzania ambapo Kamati inakaa kujadili haki ya mchezaji dhidi ya klabu kubwa na hatimaye kuamua kwa manufaa ya mchezaji, tena pasipo kupiga kura kwa misingi ya upenzi na unazi. Kamati ya Mwanasheria Mashuhuri na mwenye Msimamo Bw. Richard Sinamtwa iliamua kustafsiri kanuni kwa kufuata ushahidi uliopo na kwa haki kabisa pasipo kujiingiza katika mtego wa kupiga kura kama ambavyo tumekua tukiiona huko nyuma.

PILI: Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti ilitumia busara ya hali ya juu kwa kukataa ombi la Yanga la kutengua uteuzi wa Bw. Hans Pope katika Kamati hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga ilileta hoja ya kumkataa Bw. Hans Pope kwa misingi ya mgongano wa kimaslahi na kumtaka mwenyekiti atoe uamuzi juu ya suala hilo. Endapo mwenyekiti angetoa maamuzi ya kumuondoa Hans Pope, basi angejiingiza katika uvunjaji wa Katiba ya TFF kwasababu yeye sio mamlaka ya uteuzi wa Hans Pope katika Kamati hiyo. Mwenye mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo Yanga walipaswa kuelewa hilo na si kuishinikiza kamati, hususan Mwenyekiti, amuondoe Hans Pope kwenye Kikao.

TATU: Maamuzi ya Kamati yamefungua njia kwa wachezaji wengi ambao mikataba yao inachezewa na vilabu kwa muda mrefu pasipo kuwa na nafuu yoyote ya kisheria kwa wachezaji hao ambao ndio nguzo ya muhimu katika mpira wa Tanzania. Hata hivi sasa kuna wachezaji ambao bado hawajalipwa stahili za mikataba yao ndani ya Yanga. Tunawaomba wajitokeze ili tuwasaidie wapate haki zao za kisheria kama ambavyo imetokea kwa Okwi.

NNE: Pamoja na madai ya Yanga ya kukata rufaa FIFA / CAS, naomba wajue kuwa haki yao ya kukata rufaa inatokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF imetekeleza wajibu wake. Uamuzi huo wa Kamati umejenga msingi muhimu sana katika suala zima la kuheshimu na kutekeleza mikakaba kwa mujibu wa kanuni za FIFA. Endapo Yanga watakata rufaa kama wanavyodai, itakuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha nguzo ya kuheshimu mikataba ya wachezaji inapewa msisitizo unaostahili.

MGOGORO KATI YA YANGA NA OKWI
Mkataba wa Yanga na Okwi, ambao ulisainiwa tarehe 12 Disemba 2014 umekuwa na mapungufu yafuatayo:
1.Mkataba huo umempa majukumu mchezaji kufuatilia ITC na suala zima la yeye kupata vibali vya kucheza. Hii ni kinyume na Kanuni za FIFA ambao zinatamka bayana kuwa jukumu la kufuatilia ITC ni la wanachama wa FA, lakini Yanga walimtwisha Okwi zigo hilo. Okwi alitekeleza jukumu hilo.
Kamati ililiona hilo na kusema wazi kuwa hilo sio sahihi. Ni vema wachezaji wajue kuwa hilo sio jukumu lao.
2.Pili Yanga, kwa mujibu wa mkataba, walikuwa na haki ya kumkata mchezaji theluthi moja ya mshahara wake wa mwezi endapo atakosa mechi tatu au zaidi. Yanga walimkata Okwi Mishahara ya miezi mitano, kinyume na matakwa ya mkataba na pasipo maelelzo yoyote.
3.Yanga na Okwi walikubaliana kuwa mchezaji atalipwa ada ya kusaini mkataba (signing on – fee) ya US$ 100,000, kwa Awamu mbili. Awamu ya kwanza wakati wa kusaini mkataba na awamu ya pili tarehe 27 Januari 2014. Mpaka hivi sasa, Yanga wamelipa US$ 50,000 tu na bado kuna deni la US$ 50,000. Huu ni uvunjaji wa mkataba wa wazi kabisa.
4.   Kipindi chote mchezaji akiwa na klabu ya Yanga, hajapewa nyumba kama ambayo walikubaliana. Huu ni ukiukwaji mwingine wa mkataba.

Baada ya Okwi kuanza kudai haki zake tajwa hapo juu, Yanga waliamua kutomlipa mteja wetu mishahara ya miezi mitano kinyume na matakwa ya mkataba kati yao.

MPANGO WA SIRI WA YANGA
Yanga walikuwa na mpango wa siri wa kuvunja mkataba na Emmanuel Okwi ili wamkomoe mteja wetu, ashindwe kucheza mpira, kiwango chake kiporomoke na itumike kama onyo kwa wachezaji wengine ambao wanadai haki zao. Mpango huu ulitekelezw kama ifuatavyo:

a.Tarehe 27 Juni 2014, Yanga waliandika barua kwenda TFF, ikiitaka TFF, pamoja mambo mengine, itambue kuwa mkataba kati yao na Okwi umefutwa. Barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
b.Tarehe 25 Julai 2014, Yanga waliandika barua ya pili kukumbushia barua yao ya tarehe 27 Juni 2014. Barua hiyo ya pili haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
c.Tarehe 20 Agosti 2014 Yanga waliandika barua nyingine tena wakikumbushia hoja zao tajwa hapo juu. Kwa mara ya tatu, barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
d. Yanga waliandika barua nyingine ya nne tarehe 25 Agosti 2014 ikiwa na hoja zile zile za kusitisha mkataba na mteja wetu. Kwa mara ya nne barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.

Baada ya TFF kupanga tarehe ya kikao cha Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji na kutoa barua ya wito tarehe 27 Agosti 2014 ndipo kwa mara ya kwanza mchezaji Emmanuel Okwi akafahamu kuwa Yanga wameomba kuvunja mkataba wake.

Tarehe 27 Agosti 2014, Emmanuel Okwi aliiandikia Yanga KUKUBALI ombi lao la kuvunja mkataba.
Mosi, Kama Mkataba ulikuwa ni kati ya Yanga na Okwi, ni kitu gani kiliifanya Yanga ishindwe kumpa angalau nakala ya barua nne ambazo ilizipeleka TFF?

Pili, Wakati Yanga wanaomba kuvunja mkataba, walikuwa wameshamlipa Okwi stahili zake kwa mujibu wa Mkataba huo?

Tatu, Je visingizio vya kuvunjwa kwa mkataba wa Okwi vina uhusiano na idadi ya majina ya wachezaji wa kigeni wa Yanga?

Ni bayana kuwa Yanga walitafuta kila aina ya kisingizio ili mteja wetu aonekane kuwa ndio amevunja mkataba wakati ni wazi kuwa Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja mkataba huo tarehe 27 Januari 2014 kwa kushindwa kumlipa mteja wetu US$ 50,000 za ada ya kusaini mkataba.

HOJA MBELE YA KAMATI
Mbele ya Kamati Yanga walileta hoja kuwa: Hans Pope ana mgongano wa maslahi kwa kuwa amemsajili Okwi Simba na yeye ni mjumbe wa Kamati hii; Okwi amekataa kuongeza au kupunguza mkataba kama ilivyopendekezwa na Yanga; Okwi ameleta madai yasiyo na msingi ya kutaka apewe nyumba ya kuishi; hajacheza mechi 6 hivyo kuikosesha Yanga ubingwa. Okwi amefanya makubaliano na Klabu ya Wadi Geldi ya Misri wakati ana mkataba na Yanga. Hivyo basi Yanga waliitaka Kamati itamke kuwa mkataba kati yao na Okwi umesitishwa, imfungie Okwi kucheza mpira Tanzania Maisha na ailipe Yanga dola za kimarekani laki mbili.

Tukimwakilisha Okwi, tulitoa hoja kuwa: Mteja wetu amekubali ombi la Yanga la kuvunja mkataba ambalo limo katika barua zake nne; Yanga ndio wamevunja mkataba kwa kushindwa kulipa signing fee US$ 50,000; Mishahara ya miezi mitano US$ 15,000 na kodi ya nyumba US$ 2,800. Madai hayo ni kwa mujibu wa mkataba.

Baada ya Maswali toka kwa Kamati kwa pande zote mbili, Yanga waliomba kufuta barua zao, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na kamati.

Kamati, hatimaye ilifanya maamuzi ya kihistoria katika kulinda haki za kimkataba za wachezaji kama ambayo imeelezwa hapo juu.Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, anapaswa kuipongeza kwa dhati kamati kwa maamuzi ambayo wanajenga mpira wa nchi hii. Vilabu vinapaswa kufahamu kuwa haki za mchezaji lazima ziheshimiwe.

Hoja za Yanga kuwa hakukuwa na madai ya fedha sio sahihi kwasababu Majibu toka kwa Okwi na mabishano ya maneno mbele ya kamati hiyo ilijadili kwa kina madai ya fedha ya Okwi na hata Yanga walikiri kutolipa madai hayo. Hivyo basi si sahihi kusema kuwa eti suala la madai ya fedha halikujadiliwa. (ona kiambatisho MNA1)

Msingi wa malalamiko ya Yanga ni barua ya tarehe 27 Juni 2014, ambayo hakuna sehemu ambayo inatamka suala la Simba. Kama kuna kesi dhidi ya Simba, wasubiri wakati wa kupitia pingamizi za usajili lakini suala ambalo Yanga walilalamikia ni kusitisha mkataba na Okwi na madai ya fidia.

Kamati ya Sheria na Mwenyekiti wake hawana mamlaka ya kujadili uteuzi au uwepo wa Hans Pope kwenye kikao hicho. Mamlaka ya Uteuzi ndio, kwa mujibu wa katiba ya TFF, yenye uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo.

Kwakuwa rufaa ni haki ya kila mtu, Uamuzi wa kukata rufaa Fifa / CAS ni haki ya kisheria lakini tuwakumbushe Yanga kuwa “UKITAKA HAKI, TENDA HAKI KWANZA”.

DK. DAMAS DANIEL NDUMBARO (PhD)
Maleta & Ndumbaro Advocates

Muwakili wa Mchezaji

Monday, September 8, 2014

KOCHA PATRIC PHIRI ASEMA KIKOSI KIPO KAMALI KWA VPL

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba  Patrick Phiri amesema amelizishwa na kiwango cha timu hiyo mara baada ya kuitandika timu ya Gor mahia kutoka Kenya  kwa mabao 3 kwa 0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi.
Akizungumza na mkali wa dimba tz.blogspot.com Patrick Phiri  amesema kuwa wachezaji wake wanajituma katika michezo yao na kucheza vizuri katika mechi zote anazoziongoza.

Phiri amesema wanacheza vizuri uwanjani,uwezo umeongezeka,wamecheza na timu bora kutoka kenya,kwa hiyo naweza kusema hiki ni kipimo sahihi kwa timu yangu"alisema Patrick Phiri 

Patrick Phiri amesema maandalizi waliyoyafanya visiwani Zanzibar kumewafanya wachezaji wake wawe vizuri na anafuraha kuona kikosi chake kimeimalika.

YANGA YASEMA KUFA NA KUPOMA KUHUSU SAKATA LA OKWI KUKATAA RUFAA FIFA YASEMA MPAKA KIELEKE

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji  kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.
Mwenyekiti wa Kamati  ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslah.

                                              MAAMUZI YA KIKAO CHA JANA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7
mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.

Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.

Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.

Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo,hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.

Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.

Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.

Hata hivyo mjumbe huyo hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi. Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.

Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.
Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.

Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.

Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi watakapolipa.

Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.