Timu ya Ashanti United iliyopanga ligi kuu msimu huu inatarajiwa kufanya ziara mkoani Kigoma, maarufu kama Brazil ya
Tanzania kujiandaa na msimu, mara tu baada ya kurejea Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
Kigoma inaitwa Brazil ya Tanzania kwa
sababu ya kuibua nyota wengi wa soka, kuanzia enzi za akina Sunday Manara,
Athumani Juma Kalomba (marehemu), Abedi Mziba, hadi sasa akia Juma Kaseja.
Ashanti itaondoka Dar es Salaam Jumanne
na itakuwa Kigoma kwa takriban wiki mbili ikijifua na kucheza mechi za kujipima
nguvu na timu mbalimbali za huko.
Timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, imekuwa ikijifua mjini Dar es Salaam kwa takriban mwezi mzima na kucheza mechi kadhaa za kujipima nguvu.
Timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, imekuwa ikijifua mjini Dar es Salaam kwa takriban mwezi mzima na kucheza mechi kadhaa za kujipima nguvu.
Mechi ya mwisho ilifungwa na Azam FC
mabao 5-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na sasa inakwenda
kurekebisha makosa Kigoma.
Ashanti inakumbukwa enzi zake ikicheza
Ligi Kuu muongo uliopita kwa kuibua vipaji vya nyota wengi ambao baadaye
walikuwa tegemeo la timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Miongoni mwao ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Jabu, Juma Nyosso, Said Mourad, viungo Jabir Aziz, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na wengineo.
Timu hiyo yenye maskani yake katika
soko la Ilala Boma, karibu kabisa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
inatarajiwa kuleta changamoto mpya katika Ligi Kuu, hususan dhidi ya timu
kongwe, Simba na Yanga.
Pamoja na kupandishwa Ligi Kuu na
vijana wadogo wenye vipaji, Ashanti imejiimarisha kwa kuongeza wakongwe kadhaa,
akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Said Maulid ‘SMG’ aliyekuwa
anacheza Angola. |
![]() |