TIMU ya Wagosi wa wakaya Coastal Union ya
Tanga Mabingwa ya ligi kuu mnamo mwaka 1988 inataraji kushuka dimbani kucheza mechi ya Kirafiki ya Kimataifa na Mabingwa wa soka
Uganda URA Jumatano wiki ijayo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani Tanga.
Athibtisha taarifa hizo,Mwenyekiti wa timu hiyo,Hemed Aurora "Mpiganaji"alisema ni kweli mechi hiyo ipo na kinachofanyika hivi sasa ni kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa timu hiyo ili iweze kutua mkoani hapa kwa ajili ya mchezo huo.
Aurora alisema baada ya kumalizika mechi hiyo kikosi cha timu hiyo kitaondoka mkoani Tanga kuelekea Mombasa nchini Kenya kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Bandari lengo likiwa ni kukiimarisha kikosi hicho kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu.
Licha ya kucheza na Bandari lakini pia wapo kwenye mikakati ya kuzungumza na uongozi wa Yanga ili kuweza kucheza nao mechi ya majaribio siku ya Iddi Pili kwenye dimba hilo la Mkwakwani ambapo alisema anaamini mazungumzo hayo yatafanikiwa.
Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa lengo la timu hiyo msimu ujao ni kuhakikisha wanafanya vizuri ili kuweza kurudisha heshima yao ya mwaka 1988 ya kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo na kueleza hilo linawezekana kutokana na mshikamano uliopo baina ya wapenzi,wanachama na uongozi wao.
Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo ,Meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani,Mbwana Msumari alisema kwa mara ya mwisho uwanja huo kulichezwa mechi ya kimataifa mwaka 1988 kati ya African Sports na timu kutoka nchini Swithland wakati huo African Sports ni mabingwa wa Kombe la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Msumari alisema na mwaka huo huo ,Coastal Union wakacheza na Cost De Solver ya Msumbuji ambayo ilikuwa ikishiriki mashindano ya Klabu bingwa kwa hiyo anaamini mechi hiyo itakuwa na mvuto wa aina yake kutokana na historia ya timu hiyo.