
Napoli kwasasaiajipanga kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Italia na Ligi ya Mabingwa Ulaya huku wakiwa na fedha za kutosha kutumia baada ya kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani kwenda Paris Saint Germain kwa ada ya euro milioni 64. Albion ambaye ametoka katika shule ya soka ya Valencia akiwa kama mchezaji wa kiungo aliibuka katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo mwaka 2003 wakati huo ikifundishwa na kocha wa mpya wa Napoli Rafa Benitez kabla ya kuhamia Madrid mwaka 2009 ambako muda mwingi alitumika kama mchezaji wa akiba. Pamoja na kukosa namba klabuni kwake alifanikiwa kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania katika michuano ya Kombe la Dunia 2010 na michuano ya Ulaya mwaka jana.