Club ya Yanga jioni ya leo katika Dimba la Uwanja wa Taifa Taifa Jijini DAR
kukabiliana na Timu ya inayo milikiwa na Mamlaka ya Mapato ya nchini Uganda URA
kwa mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa sare ya bao 2-2.
Sare hiyo haikuwa nyepesi, kwani
mabingwa wa Tanzania Bara walilazimika kuhaha kusaka mabao ya kusawazisha hadi
walipojitoa uwanjani salama dakika ya 90 kwa bao la Jerry Tegete.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na
refa Kennedy Mapunda aliyesaidiwa na Iddi Maganga na Othman Othman, hadi
mapumziko URA tayari walikuwa mbele mkwa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa dakika ya 42 na Litumba Yayo, ambaye jana Watoza Kodi hao wa Uganda wakiilaza Simba SC 2-1, alifunga mabao yote. Kipindi cha kwanza URA ndio waliotawala mchezo kwa kucheza kwa kasi nzuri, uelewano mzuri na kushambulia kwa nguvu, wakati Yanga SC walionekana kukosa mipango. Kipindi cha pili, URA walianza tena vyema na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 61, mfungaji Yayo tena akiweka rekodi ya kufunga mabao manne Taifa ndani ya siku mbili. Kocha Mholanzi, Ernie Brandts alilazimika kufanya mabadiliko baada ya bao hilo, akiwaingiza Haruna Niyonzima kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi wingi ya kulia, Bakari Masoud kuchukua nafasi ya Hamisi Thabit na Abdallah Mnguli ‘Messi’ kuchukua nafasi ya Shaaban Kondo. Mabadiliko hayo yaliisaidia Yanga SC ambayo iliongeza kasi ya mashambulizi na kufanikiwa kuchomoa mabao yote, moja baada ya lingine.
Mrundi Didier Kavumbangu alianza dakika
ya 66 akiunganisha krosi ya beki Juma Abdul kabla ya Tegete kusawazisha dakika
ya 90 baada ya kumzidi maarifa kipa wa URA, Yassin Mugabi.
Tegete ambaye ana muda mrefu
hajaifungia bao Yanga, alipagawa mno kwa kufunga bao muhimu leo na kwenda kushangilia
mbele ya mashabiki kwa ishara mbili- kuomba msamaha na pili kuwaambia anaipenda
Yanga kwa kuibusu nembo ya klabu iliyopo kwenye jezi sambamba na kuwapa ishara
ya kuwataka watulie, mpira hauhitaji papara.
MSHAMBULIAJI
Mniegria wa Yanga, Ogbu Brendan Chukwudi aliondolewa ghafla katika kikosi cha
kwanza cha Yanga baada ya kuumia wakati akipasha misuli moto kujianda kuingia
mchezoni dhidi ya URA ya Uganda, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Deo
Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir 14, Salim
Telela 2, Said Bahanuzi/Niyo, Hamisi Thabit 28/Bakari Masoud, Jerry Tegete,
Didier Kavumbangu na Shaaban Kondo18/Abdallah Mguli.Kocha Mholanzi, Ernie Brandts alimuondoa kabisa Chukwudi katika orodha ya wachezaji wanaoshiriki mechi ya leo na kumuanzisha Mrundi, Didier |