
Kocha mpya wa United, David Moyes
ametanabaisha kuwa angependa kuwasajili wote.
kiungo wa Barcelona na mshambuliaji wa
Kipoland wa Borussia Dortmund katika klabu yake kabla ya kikosi chake
hakijakwenda katika ziara ya Asia na Australia katikati ya mwezi ujao.
Inafahamika kwamba, wachezaji wote hao
wameonyesha nia zao za kuhamishia cheche zao kwa mabingwa hao wa Ligi
Kuu ya England, hivyo United wanaweza kufanikisha dili hizo.

Robert Lewandowski
Klabu yake ya zamani Fabregas, Arsenal
haijaonyesha nia na malengo ya kumsajili tena iwapo mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 26 ataondoka Nou Camp, lakini United inafahamika wanamtaka kwa
dhati kiungo huyo aliyeichezea kwa miaka nane timu hiyo ya London kabla
ya kurejea Hispania miaka miwili iliyopita.

Lewandowski anaweza kuhamia England baada ya matumaini yake kuhamia kwa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich kukatwa wiki hii.
United wamekuwa wakimfuatilia
mshambuliaji huyo wa Poland kwa miezi kadhaa na wanaamini anaweza
kuzalisha ushindani mzuri kwa Robin van Persie, ambaye atatimiza miaka
30 muda mfupi kabla timu haijaanza kutetea ubingw awake Agosti.
Changamoto: Robin van Persie anaweza kukabiliana na changamoto kubwa mwanzoni mwa msimu ujao Man United
Kuwasili kwake pia kunaweza kukuza
shinikizo kwa Wayne Rooney ambaye ameomba kuondoka Old Trafford tangu
mwishoni mwa msimu uliopita.