MSHAMBULIAJI Wayne Rooney atatakiwa
kuwasilisha barua ya maandishi ya kuomba kuondoka ikiwa anataka kuachana
na Manchester United.
Mpachika mabao huyo wa Old Trafford,
alirejea mazoezini jana huku mustakabali wake ukiwa bado haueleweki.
Imefahamika hakuwa na Mkutano mahsusi na kocha mpya David Moyes juu ya
suala lake.
Hilo linaweza kutokea katika kituo cha
mazoezi cha klabu, Carrington leo. Wawili hao walizungumza jana, lakini
si kwa muda mrefu na msimamo wa United kwake bado haujabadilika.
Hajielewi: Mustakabali wa Wayne Rooney bao haueleweki licha ya jana kurejea mazoezini
Wamesema mshambuliaji huyo wa England
hauzwi. Kuhusu tetesi za wapinzani wao katika Ligi Kuu, Arsenal kutaka
rasmi kumsajili tangu wiki iliyopita, United bado haijawasiliana na
yoyote anayemtaka Rooney.
Sakata hili linaweza kugeuka tu iwapo
mshambuliaji mwenyewe ataamua kulazimisha kuondoka. BIN ZUBEIRY
iliandika mwishoni mwa msimu uliopita kwamba, Rooney aliomba kuondoka
kwa kocha aliyestaafu, Sir Alex Ferguson.
Ombi la kuondoka litamaanisha Rooney
hatadai chochote katika Mkataba wake wa miaka miwili uliobakia ambao
alikuwa analipwa Pauni 250,000 kwa wiki.
Huku Moyes akitarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza kesho, ufafanuzi utakuja muda si mrefu.
Wakati huo huo, mchezaji mwenzake wa
zamani Rooney, Mreno Cristiano Ronaldo ameendelea kuweka wazi juu
mapenzi yake na United. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amesema jana
kwamba anataka kurudi Ligi Kuu, lakini hakusema lini.
"Nalikosa kweli soka la England. Kwangu
ilikuwa moja ya miaka bora katika maisha yangu ya soka wakati nipo huko
Manchester United. Ni klabu ambayo bado ipo moyoni mwangu. naikosa kweli
kweli. Lakini kwa sasa maisha yangu yapo Hispania. Nafurahia kucheza
huko pia. Mustakabali hatuwezi kuujua,"alisema Ronaldo.