Tuesday, July 9, 2013

THIERRY HENRY NAYE YUMO KIKOSI CHA WACHEZAJI 10 WA MLS

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry ni moja kati ya wanadinga nyota 10 watakaounda kikosi kutoka katika Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS ambacho kitapambana na AS Roma ya Italia Julai 31 huko jijini Kansas. Henry mwenye umri wa miaka 35 mshambuliaji wa klabu ya New York Red Bull ambaye aliisadia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia mwaka 1998, amefunga mabao sita katika mechi 17 alizoichezea timu hiyo msimu huu. Kabla ya kwenda Marekani mwaka 2010 akitokea klabu ya Barcelona, henry amewahi kucheza katika vilabu vya Juventus na Arsenal. Golikipa wa FC Dallas ambaye ni raia wa Peru Raul Fernandez, kiungo wa timu ya taifa ya Canada Will Johnson na Beki wa Kansas City Aurelien Collin ambaye ni raia wa Ufaransa ni miongoni mwa wachezaji wasiokuwa raia wa Marekani walioteuliwa katika kikosi hicho cha nyota wa MLS.

FIFA-SEPP BRATTER ATARAJI KUZUNGUMZA NA MAOFISA WA ISRAEL

Bratter akiyatafakari mazungumzo
Sepp Blatter rais wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA amemweleza kiongozi wa michezo nchini Palestina kuwa atazungumza na maofisa wa Israel ili kujaribu kuondoa vizuizi vya kusafiri walivyowekewa wachezaji wa taifa hilo. Blatter alitarajiwa kukutana na ofisa mkuu wa soka nchini Israel kabla ya kuzungumza na kiongozi wa kisiasa wan chi hiyo waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuzungumzia suala hilo. Palestina wamekuwa wakichukizwa na vikosi vya usalama vya Israel ambavyo vinalinda mji wa Gaza kuwazuia wanamichezo wa taifa hilo kusafiri kwa uhuru katika pande hizo mbili. Blatter amesema atakwenda Israel sio kwenda kukitetea Chama cha Soka cha Palestina lakini pia kutetea misingi ya kanuni za FIFA ambayo ni kuunganisha watu na sio kuwagawa.

MESSI RASMI ATARAJIWA KUREJEA BARCA MAZOEZINI JULAI 15

Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa argentina na club ya fc Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kurejea mazoezini Julai 15 baada ya kupumzika kwa wiki moja pekee katika likizo yake kutokana na majukumu mbalimbali ambayo yamekuwa yakimtinga. Masimu wa 2012-2013 kwa mchezaji huyo nyota ulimalizika Juni 15 baada ya Argentina kuigaragaza Guatemala kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, hivyo kumanisha kwamba nyota huyo angekuwa na mwezi mzima wa kupumzika kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Hata hivyo Messi mwenye umri wa miaka 26 alitumia nafasi hiyo kucheza mechi mbalimbali za hisani kuzunguka dunia na kumaliza ziara yake hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita huko Chicago, Marekani. Jumla ya ziara zote hizo Messi amesafiri kilimita zaidi ya 90,000 toka msimu wa ligi ulipomalizika akitembelea nchi za Argentina, Ecuador, Guatemala, Italia, Senegal, Colombia, Peru na Marekani. Nyota huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya msuli mwishoni mwa msimu uliopita na mapumziko mafupi aatakayopata yatawapa uhakika mdogo madaktari juu ya afya yake kabla ya kuanza msimu mpya wa 2013-2014.

ROLNADO NAYE KUWANIA TUZO YA UNYAYO WA DHAHABU:

Mshambuliaji nyota mahiri wa club ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa katika orodha ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya kiatu cha Dhahabu kwa mwaka 2013. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa ureno atakuwa mchezaji wa kwanza wan chi hiyo kushinda tuzo hiyo ambayo ilianza kutolewa mwaka 2003 mahsusi kwa wachezaji waliozidi umri wa miaka 28. Mchezaji mwenzake wa Madri Iker Casillas na kiungo mahiri wa Barcelona Andres Iniesta ni miongoni wa nyota wengine walioteuliwa kugombea tuzo hiyo. Wachezaji waliwahi kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa kuangalia uwezo wake wa kipindi chote alichocheza soka na kiwango chake cha sasa, ni pamoja na Roberto Carlos, Ronaldinho, Francesco Totti na mshindi wa mwaka uliopita Zlatan Ibrahimovic. Wachezaji wanaweza kushinda tuzo hiyo mara moja pekee, ambapo sherehe zake hufanyika jijini Monaco kila mwaka toka ilipoanzishwa. Mbali na hao wengine waliokuwemo katika orodha ya mwaka huu ni pamoja na Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala, Andrea Pirlo anayekipiga Juventus, Didier Drogba kutoka Galatasaray, Frank Lampard-Chelsea, Miroslav Klose-Lazio, David Trezeguet-River Plate and David Beckham-Paris Saint-Germain.

Sunday, July 7, 2013

STEWART HALL AMKUBALI KASEJA ASEMA BADO NI BONGE LA KIPA TZ"

Stewart hall akitabasamu kwa pozi la aina yake
Muingereza Stewart Hall Kocha  Mkuu wa Azam FC"bila kupepesa macho ametanabaisha kuwa Kaseja anastahili kuitwa tanzania one kutokana kuwa bado anauwezo mkubwa wa kulinda lango" Hall ameweka wazi na kusema kuwa kwa sasa sina mpango wa kusajili kipa mwingine kutokana na makipa niliyokuwa nao ambao ni Aishi Manula na Mwadini Ally" nataka hawahawa wapambane kuwania nafasi ya kipa namba moja wa azam fc" hivyo kwa msisitizo amesema sina mpango wa kusajili kipa mwingine.
Hall amesema kipa wake mwingine "Jackson Wandwi anafikiria kumpeleka kucheza kwa mkopo katika Club ya Ashanti United ya Ilala iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ili kupata uzoefu baadaye arejee kushindana na Mwadini na Aishi.
Aidha Hall amesema nafahamu fika kuwa Kaseja ametupiwa virago MSimbazi na nasikia watu wanamzungumzia sana wakimhusisha na Azam fc. Mimi nakubali yule ni kipa mzuri na ana uzoefu. Ila mimi nina makipa wazuri wawili, Aishi na Mwadini. Nataka hawa washindane ili kumpata kipa nambari moja wa timu"
Hata hivyo Hall amesema kuwa bado Azam ina makipa wengine wazuri wa timu za vijana, ambao watakuwa wakipewa nafasi ya kujifua na kikosi cha kwanza msimu ujao.
“Hivyo nitakuwa na Aishi na Mwadini kama makipa wawili imara wa timu ya kwanza, maana yake Wandwi ataendelea kupoteza kiwango chake. hivyo nifikiria bora nimpeleke Ashanti ili akakuze kipaji chake na kupata  uzoefu, baadaye arejee kwenye timu akiwa imara zaidi".
Mbali na hilo tulipomuuliza kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara na michuano ya kombe la shirikisho barani afrika Hall amesema kwamba Azam ambayo itaipeperusha bendera ya Tanzania kwa mara ya pili mfululizo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, iko katika mazoezi.
“Tunaendelea na mazoezi ya msimu mpya. Kwa sasa tupo katika programu ya ufukweni na gym. Baada ya hapo tutaanza programu rasmi ya uwanjani. Lakini wiki mbili za mwanzo za Agosti tutakwenda Afrika Kusini kuweka kambi,”.

MARION AFANIKIWA KUTWAA TAJI LA KWANZA LA MICHUANO YA GRAND SLAM.

Marion Bartoli mwanadada nyota katika tenisi,  amefanikiwa kushinda taji lake la kwanza la michuano ya Grand Slam baada ya kumchalaza Sabine Lisicki wa Ujerumani kwa seti 6-1 6-4 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon. Bartoli ambaye anashika namba 15 katika orodha za ubora kwa upande wanawake alitumia dakika 30 pekee kushinda seti ya kwanza wakati mpinzani wake Lisicki akionekana kushindwa kumudu vishindo katika fainali yake ya kwanza ya Grand Slam. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Bartoli amesema haamini kama amenyakuwa taji hilo na alikuwa akijisikia kucheza kwa kiwango chake cha juu huku kila kitu alichofanya kikimuendea sawa. Michuano hiyo inaendelea tena baadae kwa mchezo wa fainali kwa upande wa wanaume ambapo Andy Murray wa Uingereza anayeshika namba mbili katika orodha za ubora atachuana na Novak Djokovic wa Serbia anayeshika namba moja katika orodha za ubora.

HISPAIN YATOLEWA NJE MASHINDANO YA VIJANA FIFA U-20" LEO GHANA VS CHILE

FIFA_WORLD_CUP_U-20_TURKEY_LOGOKatika  mechi ya jana iliyokuwa na upinzani wa hali ya juu kati ya Hispain vs Uruguay "dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa sare ya 0-0 "Ndipo Refa wa mtanange huo akamuru kuongeza dakika  30 za Nyongeza.
Thiago_AlcantaraHivyo katika dakika hizo 30 za nyongeza kunako dakika 103 ya mchezo Felipe Avenatti aliipatia Uruguay bao muhimu la kuongoza kwa njia ya Kichwa"ambapo bao hilo 1-0 limeiwezesha Uruguay kuibwaga Hispain na kufanikiwa kutinga hatua Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya Miaka 20, U-20, yanayochezwa huko Nchini Turkey.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
MATOKEO MENGINE"
ROBO FAINALI
France 4 Uzbekistan 0
Magoli:
*Yaya Sanogo (dk31')
*Paul PogbaP (dk35' Penati)
*Florian Thauvin (dk43' Penati)
*Kurt Zouma (dk64')
Uruguay 1 Spain 0
Goli:
*Felipe Avenatti (dk103’)
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Hivyo sasa kwa ushindi huo Uruguay katika hatua ya Nusu Fainali watashuka dimbani kupepetana na Mshindi wa Mechi ya Iraq vs South Korea.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
RATIBA ROBO FAINALI  LE; JULAI 7
[Saa 12 Jioni]
Kayseri
Iraq v South Korea
[Saa 3 Usiku]
Istanbul
Ghana v Chile
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Katika Robo Fainali nyingine iliyochezwa jana Timu ya Taifa ya France ilifanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuilaza Uzbekistan kwa Bao 4-0 hivyo sasa kwa matokeo hayo France itacheza na Mshindi kati ya Ghana vs Chile.
Bao za France zilifungwa na Yaya Sanogo, Paul Pogba, Florian Thauvin naKurt Zouma.
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
06/07 France 4 Uzbekistan 0
06/07 Uruguay 1 Spain 0
07/07 muda 18:00 Iraq v South Korea
07/07 muda 21:00 Ghana v Chile
NUSU FAINALI
10/07 18:00 Bursa France vs Ghana or Chile
10/07 21:00 Trabzon Uruguay vs Iraq or South Korea
MSHINDI WA TATU
Tarehe 3/07 18:00  Uwanja Istanbul  Kulingana na matokea
FAINALI
Tarehe 13/07 21:00  Uwanja Istanbul
World Youth Championship{Bingwaaaaaa}
TUKUMBUKE WASHINDI WALIOPITA:
2011  Brazil
2009  Ghana
2007  Argentina
2005  Argentina
2003  Brazil
2001  Argentina
1999  Spain
1997  Argentina
1995  Argentina
1993  Brazil
1991  Portugal
1989  Portugal
1987  Yugoslavia
1985  Brazil
1983  Brazil
1981  Germany
1979  Argentina
1977  U.S.S.R.