Tuesday, July 23, 2013

FC BARCA YATARAJI KUMTANGAZA MARTINO KUWA KOCHA MPYA

Gerardo Martino ambaye ni raia wa Argentina,Kocha wa Newell’s Old Boys ya huko Argentina, anatarajiwa kutangazwa kuwa Kocha mpya wa FC Barcelona kuchukua nafasi iliyoachwa wazi Tito Vilanova kutokana na sababu za  kiafya.
Martino, mwenye Miaka 50, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na kutangazwa rasmi baadae Wiki hii.
WASIFU WAKE:
JINA: Gerardo Daniel Martino
KUZALIWA: Novemba 20, 1962 (Miaka 50), Rosario, Argentina
TIMU ya VIJANA: Newell's Old Boys
KLABU:
1980–1990  Newell's Old Boys Mechi 392  Magoli: 35
1991 Tenerife Mechi 15 Goli: 1
1991–1994  Newell's Old Boys Mechi: 81 Goli: 2
1994–1995   Lanús Mechi 30 Goli 3
1995 Newell's Old Boys Mechi 15
1996 Barcelona SC Mechi 5
ARGENTINA: Mechi 1
UMENEJA:
1998 Brown de Arrecifes
1999 Platense
2000 Instituto
2002–2003   Libertad
2003–2004   Cerro Porteño
2005 Colón
2005–2006   Libertad
2006–2011   Paraguay
2012–2013   Newell's Old Boys
2013-           Barcelona FC
Gerardo Martino akiwa Fc Barcelona atakuwa pamoja na Wasaidizi wake mwenyewe ambao ni Elvio Paolorrosso, Kocha wa Viungo, na Msaidizi Jorge Pautasso.
Awali ilitegemewa Kiungo wa zamani wa Barca, Luis Enrique, ndie atatwaa madaraka Nou Camp lakini tatizo kubwa ni kuwa Enrique alijiunga na Klabu ya La Liga Celta Vigo Mwezi uliopita tu na ukaja utata wa Mkataba.
Martino, au ‘Tata’ kama alivyo maarufu, anakuwa Muargentina wa nne kuwa Kocha wa Barcelona wengine ni Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti na anatua Nuo Camp kuungana na Supastaa wa Argentina Lionel Messi ambae amemsifia sana Kocha huyu.
Jumatano, Barcelona inacheza Mechi ya Kirafiki na Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich na itakuwa chini Jordi Roura kwenye Mechi hiyo iatakayochezwa huko Allianz Arena, Munich.

CHELSEA YAJIPANGA KUTUMA DAU LA PILI KUHUSU ROONEY

CHINI ya kocha mpya Jose mourinho club ya Chelsea ipo tayari kutuma ofa ya pili ya kumsajili Wayne Rooney. 
Kocha wa Stamford Bridge, Jose Mourinho bado anakaza masuli kumpata mshambuliaji wa Manchester United na ananiandaa kulipa Pauni 30 kukamilisha dili hilo. 
Chelsea iliwasilisha ofa ya awali wiki iliyopita, lakini ikakataliwa na klabu ya Old Trafford.

Jamaa huyu hatabiriki yupo mbioni kutimka
United ilikataa pofa ya Pauni Milioni 23 taslimu jumlisha Milioni 2.5 malipo ya ziada ikisistiza Rooney, mwenye umri wa miaka 27, hauzwi.
Chelsea inafurahi kumpa mshahara wa Pauni 240,000 Rooney kwa wiki anazolipwa United na watampa Mkataba wa miaka mitano kama atafanikiwa kulazimisha kuondoka kwa mabingwa hao wa England.
Rooney ambaye mambo yake hayajaeleweka anafanya mazoezi viwanja vya mazoezi vya United, Carrington baada ya kurejea kutoka kwenye kambi ya klabu kujiandaa na msimu kwa sababu ya kuumia nyama.
Lengo kuu: Jose Mourinho anataka kumnasa Wayne Rooney ili kuimarisha safu ya ushambuliai ya Chelsea
Kazi kweli: Mustakabali mzito wa Rooney unampa wakati homa David Moyes katika siku zake za mwanzo kazini United
 
Kocha wa United, David Moyes ameendelea kusistiza Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika mkataba wake Old Trafford, hauzwi.
Lakini anaweza kupambana sana kumbakiza mchezaji huyo, kwqa sababu Mourinho anamtaka kweli Rooney na anapambana kumpata.

Monday, July 22, 2013

PUYOL ASEMA TITO VILANOVA AMEWEKA PIGO KWA BARCA

Nahodha wa club ya Fc Barcelona, Carles Puyol amesema kuwa uamuzi wa Tito Vilanova kuachia ngazi kuinoa klabu hiyo kuwa ni pigo kubwa. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alitangaza kuachia ngazi wiki iliyopita ili zweze kuendelea na matibabu yake ya saratani baada ya kuiongoza Barcelona kunyakuwa taji la La Liga katika msimu wa 2012-2013.
Puyol amekiri kuwa habari ya kujizulu kwa Vilanova imekuja kwa mshituko lakini ameahidi kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu ujao ikiwa kama sehemu ya kumshukuru kocha huyo. Beki huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akisumbuliwa na majeruhi amedai kuwa wakati Vilanova akiwaaga aliwaomba kujituma kwa bidii katika msimu mpya uliopo mbele yao na watafanya hivyo kwa heshima yake.

UONGOZI WA URA YA UGANDA YAJIA JUU SIMBA KUHUSU OWINO"

URA ya Uganda kupitia uongozi wake umeamua kujajuu na kusema unashangazwa na kuiona inamtaka beki Joseph Owino.
Meneja wa URA, Sam Okabo amesema Simba walimuona mchezaji huyo hana thamani wakati akiwa mgonjwa.
Simba ilimuacha Owino ikiwa ni siku chache baada ya kubadilishana na Uhuru Selemani ambaye alikwenda Azam FC.
Lakini ikaonekana alikuwa hajapona vizuri hivyo viongozi wa Simba wakaamua kuachana naye na kuanza kuhaha kusaka mabeki wengine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope alimfuata Owino baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya URA ambayo Msimbazi walilala.

DAVID MOYES ATHIBITISHA KUHUSU CLUB HIYO KUTUMA OFA YA PILIM KUHUSU FABRIGAS

Mrithi wa Sir Alex Ferguson Meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes amethibitisha kuwa klabu hiyo imetuma ofa nyingine kwa ajili ya kujaribu kumsajili Cesc Fabregas na kuonya kuwa bado hajakata tamaa na kiungo huyo wa Barcelona. Akihojiwa na waandishi wa habari katika Uwanja wa Nissan jijini Yokohama, Japan, Moyes amesema ofisa mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward bado anafanya mawasiliano na Barcelona kuhusiana na Fabregas baada ya kutuma ofa ya pili inayokadiriwa kufikia paundi milioni 30 ambayo itakuwa rekodi mpya ya klabu kwenye usajili. 
Moyes amedai kuwa ingawa wana wachezaji kadhaa ambao wako katika mipango yao kama usajili wa Fabregas ukishindikana lakini kwasasa bado hawajakata tamaa ya kupata saini ya nyota huyo. United kwasasa wako katika ziara yao ya tatu jijini Tokyo ambapo tayari nyota wake Shinji Kagawa, Ashley Young na Chris Smalling wameshaungana na wenzake baada ya kupona

MESSI AMPIGIA UPATU KOCHA MPYA MARTINO KUCHUKUA MIKOBA YA VILANOVA

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya argetina Lionel Messi amempigia upatu kocha Gerardo Martino kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo. Baada ya nafasi ilikuwa wazi kutokana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tito Vilanova kulazimika kuachia ngazi kutokana na maradhi ya saratani yanayomsumbua. 
Martino ambaye aliiongoza timu ya Old Boys kushinda taji la Ligi Kuu chini Argentina msimu uliopita ni mmoja wa makocha wanaoewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Vilanova na Messi ana imani kuwa kocha huyo anastahili nafasi hiyo. Messi alidai kuwa Martino ni mmoja wa makocha wenye kiwango cha juu na kila mtu anamheshimu hivyo haoni tatizo kama akikabidhiwa mikoba ya kuinoa Barcelona.

MOURINHO AMPASHA DAVID MOYES KUSAHAU KUMNASA C.RONALDO

The spesho one Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemhabarisha meneja wa Manchester United, David Moyes kusahau ndoto zake za kujaribu kumrejesha Cristiano Ronaldo Old Traford. Kuna tetesi kuwa United wako katika harakati za kujaribu kumrejesha nyota huyo wa kimataifa wa Ureno pamoja na meneja mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti kusisitiza kuwa hawatamuuza. Lakini Mourinho ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa klabu hiyo amedai kuwa hadhani kama Madrid wanaweza kumruhusu Ronaldo kuondoka kwasababu ya uwezo mkubwa wa kifedha walionao kwasasa. Mourinho amesema Madrid ni klabu tajiri duniani na hawana sababu ya kumuuza nyota huyo hivyo wanaweza kukataa ofa yoyote itakayotolewa kwa ajili ya kumchukua.