Waziri Mkuu David
Cameron pamoja na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza wamekuwa miongoni mwa
watu mashuhuri waliotoa pongezi kwa mchezaji tenisi nyota wan chi hiyo
Andy Murray kwa kunyakuwa taji la michuano ya Wimbledon. Wachezaji
nyota na watu wengine maarufu nchini humo pia walitoa pongezi zao kwa
Murray mwenye umri wa miaka 26 baada ya kuwa Muingereza wa kwanza
kunyakuw ataji la michuano hiyo toka Fred Perry alipofanya hivyo mwaka
1936, kwa kumfunga Novak Djokovic kwa seti 3-0.
Cameron ambaye alikuwepo
uwanjani kushuhudia mtanange huo alimpongeza Murray kwa kuonyesha
kiwango cha juu kwenye mchezo huo na kuweka historia mpya katika mchezo
huo nchini Uingereza. Mwandishi
wa BBC katika kasri ya kifalme nchini humo, Peter Hunt alibainisha kuwa
Malkia alimtumia ujumbe binafsi Murray kumpongeza kwa kufanikiwa
kushinda taji hilo.