Golikipa mkongwe
aliyenaswa na club ya Chelsea katika kipindi cha usajili wa majira
ya kiangazi, Mark Schwarzer ameibuka na kudai kuwa anapigania kupata
namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo msimu ujao. Akihojiwa
na waandishi wa habari katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya ya klabu
hiyo jijini Kuala Lumpur, Malaysia, Schwarzer amesema wakati
akisajiliwa na timu hiyo alijua kwamba wana makipa bora na mpambano wa
kutafuta nafasi ya kuanza utakuwa mgumu. Lakini
alidai kuwa kwa juhudi na kiwango kizuri atakachoonyesha ana matumaini
anaweza kupangwa katika kikosi cha kwanza timu hiyo msimu ujao.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema wiki iliyopita kuwa Schwarzer ataleta ushindani na hamasa kwa golikipa namba moja wa klabu hiyo Petr Cech baada ya kufanya usajili huo wa kushangaza. Schwarzer ambaye amecheza katika Ligi Kuu nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka 15 ni mmoja ya wachezaji wachache waliocheza mechi zaidi ya 500 katika historia ya ligi hiyo.