Wednesday, March 19, 2014

CHELSEA YAIZIBUA GALATASARAY 2-MTUNGI.

Club ya soka ya Chelsea imefanikiwa kuichalaza Timu ya  Galataray ya Uturuki kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye UWanja wa Stamford Bridge London.

Mabao ya Chelsea yaliwekwa kimiani  na Samuel Eto’o na beki Garry Cahill na kuipa Chelsea ushindi wa jumla ya mabao 3-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Istambul katika mechi ya kwanza.
UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

MARUDIANO MATOKEO.

Jumanne Machi 18

Chelsea FC 2 Galatasaray Spor Kulübü 0 [3-1]

Real Madrid CF 3 Schalke 1 [9-2]

RATIBA MECHI ZA LEO:

Jumatano Machi 19

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]

22:45Man United v Olympiacos CFP [0-2].

Tuesday, March 18, 2014

DROGBA KUFUMUA NYASI STAMFORD BRIDGE.

Mshambuliaji Mahiri wa Galatasaray ya Uturuki, akiwa na wenzake amefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa na Chelsea. 
Mara tu baada ya mazoezi, Drogba amesema yuko tayari kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya kikosi hicho cha Jose Mourinho katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Nimerudi tena hapa, kwangu ni sehemu bora na yenye kumbukumbu nyingi sana. Lakini kama ni mechi, niko tayari," alisema Drogba.
Katika mechi ya kwanza jijini Istambul, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Hivyo jibu litatapikana leo.
UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

RATIBA

MARUDIANO

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]

[Saa za Bongo]

Jumanne Machi 18

22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]

22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]

Jumatano Machi 19

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]

22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

31 WAITWA NGORONGORO HEROES KUIKABILI KENYA.

Wachezaji 31 wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Senegal.
Ngorongoro Heroes itakayokuwa chini ya Kaimu Kocha John Simkoko akisaidiwa na Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayochezwa kati ya Aprili 4-6 jijini Nairobi.
Kikosi kinachounda timu hiyo ambayo itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende, Zanzibar).
Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed (Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji).
Viungo ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John (Scouting- Mwanza).
Washambuliaji ni Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).

YANGA, AZAM KUUMANA VPL TAIFA

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 19 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Azam itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.
Baada ya saa 6 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 mchana.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.
Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ambapo atasaidiwa na Anold Bugado (Singida), Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam). Kamishna wa mechi hiyo Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
19
12
7
0
27
43
2
Yanga SC
18
11
6
1
29
39
3
Mbeya City
21
10
9
2
10
39
4
Simba SC
21
9
9
3
17
36
5
Kagera Sugar
21
8
8
5
3
32
6
Ruvu Shooting
20
7
7
6
-4
28
7
Coastal Union
21
5
11
5
1
26
8
Mtibwa Sugar
21
6
8
7
-1
26
9
JKT Ruvu
21
8
1
12
-13
25
10
Prisons FC
20
3
10
7
-4
19
11
Mgambo JKT
20
4
6
10
-17
18
12
Ashanti United
21
4
6
11
-18
18
13
JKT Oljoro
21
2
9
10
-16
15
14
Rhino Rangers
21
2
7
12
-14
13
RATIBA MECHI:
Jumatano Machi 19
Yanga v Azam FC
Jumamosi Machi 22
JKT Ruvu v Mbeya City
Rhino Rangers v Yanga
Kagera Sugar v Tanzania Prisons
Jumapili Machi 23
Simba v Coastal Union
Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting v Ashanti United
Azam FC v JKT Oljoro

Sunday, March 16, 2014

RATIBA MECHI ZIJAZO LIGI KUU VODACOM:KAZI IPO MARCH 19

VPL_2013-2014-FP
Jumatano Machi 19
Yanga v Azam FC
Jumamosi Machi 22
JKT Ruvu v Mbeya City
Rhino Rangers v Yanga
Kagera Sugar v T.Prisons
Jumapili Machi 23
Simba v Coastal Union
Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting v Ashanti United
Azam FC v JKT Oljoro

MATOKEO YA JANA:
Jumamosi Machi 15
Azam FC 4 Coastal Union 0
Mtibwa Sugar 0 Yanga 0
Kagera Sugar 2 Tanzania Prison 1

MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD PTS
1 Azam FC 19 12 7 0 27 43
2 Yanga SC 18 11 6 1 29 39
3 Mbeya City 21 10 9 2 10 39
4 Simba SC 21 9 9 3 17 36
5 Kagera Sugar 21 8 8 5 3 32
6 Ruvu Shooting 20 7 7 6 -4 28
7 Coastal Union 21 5 11 5 1 26
8 Mtibwa Sugar 21 6 8 7 -1 26
9 JKT Ruvu 21 8 1 12 -13 25
10 Prisons FC 20 3 10 7 -4 19
11 Mgambo JKT 20 4 6 10 -17 18
12 Ashanti United 21 4 6 11 -18 18
13 JKT Oljoro 21 2 9 10 -16 15
14 Rhino Rangers 21 2 7 12 -14 13

SUAREZ AFUNGUKA KUWA INIESTA ALISTAHILI TUZO YA BALLON D"OR MWAKA 2010

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez anaamini kuwa Andres Iniesta alistahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2010 zaidi kuliko mshindi wa tuzo hiyo Lionel Messi. Messi ambaye alishinda tuzo hiyo kwa miaka minne mfululizo, alinyakuwa tuzo hiyo mwaka 2010 mbele ya wachezaji wenzake wa Barcelona Iniesta na Xavi Hernandez pamoja na wenzake hao kunyakuwa taji la Kombe la Dunia wakiwa na timu ya taifa ya Hispania pamoja na taji La Liga wakiwa na klabu yao. Lakini Suarez ambaye ni Mhispania pekee kunyakuwa tuzo hiyo anadhani Xavi na Iniesta ambaye alifunga bao la ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia alitakiwa kuwa mbele ya Messi aliyepewa tuzo hiyo. Suarez amesema katika miaka ya karibuni Hispania imeuwa ikifanya mambo mengi muhimu na mchezaji yoyote wan chi hiyo anastahili kushinda Ballon d’Or. Nguli huyo ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 78 aliedelea kudai kuwa La Liga pia ina wachezaji wawili wa kiwango cha juu kabisa Messi na Cristiano Ronaldo lakini anafikiri mwaka ambao Hispania walitawadhwa mabingwa wa dunia Iniesta au Xavi walistahili tuzo ya Ballon d’Or.

Sunday, February 23, 2014

VPL:SIMBA HOI YALALA TAIFA 3-2 MBELE YA JKT RUVU,AZAM YATOA SARE NA PRISON


Baada ya Jana Mabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu VodacomTanzania Bara,Yanga  Sc Kuishindilia Ruvu Shooting Kipigo Bao 7-0 na kukamata uongozi wa Ligi hiyo.
Hii leo Mambo yamegeuka kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa wapinzani wao wa Jadi Simba Wekundu wa Msimbazi imekubali kipigo cha Bao 3-2 kutoka kwa Maafande wa Jkt Ruvu.
Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Mshambuliaji wake Mahiri Hamis Tambwe katika dakika ya 65 baada ya Kiemba kuangushwa katika eneo la hatari na muamuzi kuamuru mkwaju wa penalt.
Lakini mkali huyo alirejea tena wavuni kwa mara ya pili kunako dakika ya 84 baada kupekea krosi safi ya amri kiemba na kufunga bao hilo kwa njia ya kichwa.
Kwa upande wa Jkt Ruvu mabo yamepatikana katika dakika ya 13 mfungaji Hussein Bunu pamoja na Emmanuel Swita aliefunga magoli mawili kunako dakika ya 45 kwa njia ya penalt huku akiweka bao jingine katika dakika ya 53 baada ya kugongeana na Amos Mgisa.
Na huko kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Azam FC ikishuka kupepetana na Tanzania Prisons ya Mbeya matokeo azam imelazimishwa sare ya mabao 2-2.
Ligi Kuu Vodacom
RATIBA:
Jumapili Februari 23
Simba 2 v JKT Ruvu 3
Azam FC 2 v Tanzania Prisons 2
Jumatano Februari 26
Azam FC v Ashanti United
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Yanga SC
17
11
5
1
29
38
2
Azam FC
17
10
6
0
21
37
3
Mbeya City
19
9
8
2
8
35
4
Simba SC
19
8
8
2
19
32
5
Kagera Sugar
19
6
8
5
1
26
6
Coastal Union
19
5
10
4
5
25
7
Mtibwa Sugar
19
6
7
6
0
25
8
Ruvu Shooting
18
6
7
5
-4
25
9
JKT Ruvu
18
6
1
11
-14
19
10
Prisons FC
17
3
7
6
-5
18
11
Mgambo JKT
19
4
5
10
-17
17
12
Ashanti United
18
3
5
10
-15
14
13
JKT Oljoro
19
2
8
9
-15
14
14
Rhino Rangers
19
2
7
10
-11
13