Friday, May 16, 2014

BALE ASEMA RONALDO NI MTU POA SANA

Mchezaji Mahiri Gareth Bale ameweka wazi na kusema kuwa Mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ni Mtu mwema sana tofauti na baadhi ya Watu wanavyomchukulia.
Bale alijiunga Real Madrid akitokea Tottenham Mwaka Jana kwa Dau la Euro Milioni 100 likipiku Dau la Ronaldo aliponunuliwa toka Man United la Euro Milioni 94.
Hata hivyo, Bale, Raia wa Wales, amesisitiza Ronaldo alimkaribisha vyema Jijini Madrid na ametamka: “Tangu nifike hapa amekuwa Mtu wa ajabu kwa kunisaidia ndani na nje ya Uwanja. Ni Mtu mwema, anasaidia sana, na Siku zote anataka Timu ishinde lakini Watu wanaandika tofauti!”
Bale pia amekiri Luka Modric, ambae walikuwa nae Tottenham na kuhamia
Real Mwaka mmoja kabla, amekuwa mkarimu sana kwake.
Bale ameeleza: “Tulikuwa na Luka Miaka mitano Spurs na tulikuwa na uhusiano mzuri sana na hili limenisaidia nilip
okuja hapa. Yeye alitua hapa hamjuia Mtu na ilikuwa ngumu kwake. Lakini nilipokuja mimi nimemkuta yeye na nilifarijika sana.”
Bale pia amesema kuwepo kwa Watu maarufu kama kina Zinedine Zidane, ambae yupo chini ya Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, kumemwinua sana.
Mbali ya kuisaidia Real Madrid kutwaa Copa del Rey Msimu huu baada ya kufunga Bao la Pili, la ushindi na la ajabu dhidi ya Barcelona Mwezi uliopita, Bale pia ana nafasi kubwa hapo Mei 24 kutwaa Ubingwa wa Ulaya wakati Real Madrid itakapokutana na Atletico Madrid huko Lisbon, Ure
no kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIOZ LIGI.

TUPO TAYARI KUIKABILI ZIMBABWE- NOOIJ

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya mechi ya Kombe la Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
TAIFA_STARS-BORA1
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (Mei 16 mwaka huu), Nooij amesema kabla ya kuja Tanzania alikuwa akifuatilia Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo anawafahamu wachezaji wengi.
Amesema wachezaji wanaounda kikosi chake ni wenye uzoefu na mechi za kimataifa, hivyo wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, kwani wamepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye kambi iliyokuwa Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.
Nooij amesema ujio wa washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) kutaongeza morali ya kikosi chake.
Samata na Ulimwengu watawasili nchini Jumamosi mchana, saa 7.30 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo leo (Mei 16 mwaka huu) wanacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal ya huko.
Wachezaji waliopo kambini kwa sasa ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Himid Mao, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha, Ramadhan Singano, John Bocco, Elias maguli na Kelvin Friday.
Wakati huo huo, timu ya Zimbabwe (Mighty Warriors) inawasili kesho alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 27. Kesho saa 4 asubuhi (Mei 17 mwaka huu) Kocha wa timu hiyo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zinaanza kuuzwa kesho (Mei 17 mwaka huu) kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, OilCom Ubungo, Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala. Viingilio ni sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 tu.
…MDAU AAHIDI WACHEZAJI MIL 5/-
Mdau mmoja wa mpira wa miguu ambaye hataki jina lake litajwe ameahidi kutoa sh. milioni tano kwa wachezaji wa Taifa Stars iwapo wataifunga Zimbabwe katika mechi ya Jumapili.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linamshukuru mdau huyo, na linatoa mwito kwa wadau wengine wajitokeze kutoa motisha kwa Taifa Stars.
Bonasi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa wachezaji wa Taifa Stars itatolewa kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
TFF YAOMBOLEZA VIFO VYA WASHABIKI DR CONGO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- FECOFA, Omar Constant kutokana na vifo vya washabiki.
Washabiki 12 walipoteza maisha uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo kati ya TP Mazembe na AS Vita iliyochezwa kwenye Uwanja wa Tata Raphael, jijini Kinshasa.
“Tumeguswa na msiba huo mzito, tunatoa salamu za rambirambi kwako (Rais wa FECOFA), familia za marehemu pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,” imesema sehemu ya barua hiyo ya Rais Malinzi.
KOZI ZA UKOCHA LESENI A, B KUFANYIKA JUNI
Kocha a ukocha wa mpira wa miguu kwa ajili ya leseni A na B zinazotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)  zitafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 2 mwaka huu.
Ada kwa kozi zote ni sh. 300,000 ambapo wale watakaofanya ya A (equivalent) itaanza Julai 21-26 mwaka huu. Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B za ukocha za CAF.
Kwa wale watakaoshiriki kozi ya leseni B ambao ni wale wenye leseni C watakuwa na vipindi viwili. Kipindi cha kwanza ni kuanzia Juni 2-15 mwaka huu wakati cha pili kinaanza Juni 23 mwaka huu na kumalizika Juni 28 mwaka huu.
Wakufunzi wanaotambuliwa na CAF watakaoendesha kozi hiyo ni Sunday Kayuni na Salum Madadi kutoka Tanzania, na washiriki watajigharamia kwa kila kitu. Baadaye CAF watatuma Mkufunzi mwingine kwa ajili ya mitihani.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Thursday, May 15, 2014

SAMATTA NA ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI VS ZIMBABWE

RAIS wa shirikisho la soka nchini Tanzania, Jamal Malinzi imepigana kiume kuwasiliana na mwenyekiti na mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi  na taarifa njema juu ya mawasiliano hayo ni kwamba washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu watawasili jumamosi mchana kwa ajili ya mchezo wa jumapili.
SamataTaarifa za uhakika kutoka ndani ya TFF zinaeleza kuwa Rais Malinzi amethibitisha ujio wa wanandinga hao tegemeo kwa Taifa stars na kuibua matumaini ya Taifa stars kufanya vizuri kwasababu Samatta na Ulimwengu ni wachezaji mahiri zaidi kwa sasa.
Nyota hao wawili watatumiwa kwa mara ya kwanza na kocha wa Taifa stars, Mart Nooij katika mechi ya raundi ya awali kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam

TFF YASAINI MKATABA UDHAMINI SOKA LA WANAWAKE

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) hapa nchini limeendeleza kutunisha msuli baada ya jana kusaini mkataba na kampuni ya proin Promotions kwa ajili ya kudhamini mashindano ya Kombe la Taifa kwa wanawake yatakayofanyika kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Johnson Rukaza, alisema kuwa makubaliano hayo waliyoingia na TFF yatakuwa ni ya miaka miwili na yatawagharimu zaidi ya Sh.
 milioni 150 ili kufanikisha michuano hiyoRukaza alisema kuwa kupitia mashindano hayo ya Kombe la Taifa wanaamini vipaji vya wachezaji wanawake vitaonekana na baadaye kuisaidia timu ya Taifa ya jinsia hiyo (Twiga Stars) kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ambayo inashiriki.
Amesema kwamba wao wamefungua njia kudhamini mashindano hayo na wanawaomba makampuni na taasisi nyingine kujitokeza kudhamini mashindano hayo ikiwamo na vituo vya televisheni lengo likiwa ni kutangaza soka la wanawake.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alisema kuwa uongozi wake unawashukuru wadhamini hao wapya na inaahidi uongozi wake utahakikisha soka la wanawake linasonga mbele.
Malinzi amesema kwamba wanawaomba wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki mchezo huo kwa sababu utawasaidia kiafya, kupata burudani na kuinua hali zao za kichumi pale watakapofanikiwa kupata klabu za kucheza.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Lina Kessy, alisema kwamba wanaamini sasa mpira wa wanawake utacheza na jana ilikuwa ni siku ya kihistoria kwenye medani ya mchezo huo kwa upande wa wanawake.
Kessy amesema kwamba TFF na TWFA itahakikisha jitihada za kusaka wadau wengine zinaendelea ili mchezo huo uchezwe sehemu zote hapa nchini.
Amesema kwamba zaidi ya mikoa 17 inatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambayo mara ya mwisho yalifanyika mwaka 2008.

Tuesday, May 13, 2014

HASSAN DALALI AWAPA SOMO WANACHAMA WA MSIMBA SC


Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, amewapa somo wanachama wa klabu hiyo kuwa makini katika kuelekea kwenye Uchaguzi huo.
Akizungumzia hilo jijini Dar es Salaam, Dalali alisema kuwa sio wote wanastahili ku
wa viongozi wa klabu hiyo kongwe ambayo kwa sasa imepoteza hadhi yake.
Alisema alipokuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, aliweza kuwaunganisha wana Simba, hivyo kunastahili kiongozi mwingine mwenye mfano wake.
“Hii Simba sasa imepoteza hadhi na heshima yake katika nyanja ya soka, hivyo lazima apatikane kiongozi imara na mwenye uwezo wa kuitumikia usiku na mchana.
“Tunahitaji kupata viongozi makini hivyo siku ya Uchaguzi na wakati huu lazima tuwapime wagombea wote kwasababu tunawajua vizuri,” alisema.
Kwa mujibu wa Dalali, baadhi ya wagombea hawana hadhi na uwezo wa kuwa rais wa kwanza wa klabu hiyo, kutokana na fikra zao kuwa fupi.

MAN UNITED WATOLEA MACHO DIEGO COSTA WENGINE WATAFUATA

KLABU ya Manchester United imepiga hatua katika harakati zake za kusaka za kuimarisha kikosi chake baada ya kwenda kuwatazama Diego Costa na Ander Herrera mwishoni mwa wiki.
Baada ya kutolewa kwenye Kombe la FA na Swansea, kipigo ambacho ni mwendelezo wa msimu mbaya United, kocha David Moyes amesema kwamba kuna jitihada za dhati klabu hiyo ya Old Trafford kusajili wachezaji. 
Amekuwa akisaka beki wa kushoto, kiungo na mshambuliaji Ulaya mzima.
Mlengwa mkuu: Manchester United inataka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa
Flying high: Diego Costa and Atletico hit the top of La Liga after beating Malaga 1-0Diego Costa aliiwezesha Atletico kupanda kileleni mwa La Liga baada ya kuifunga Malaga 1-0

Msaka vipaji mkuu wa United, Robbie Cooke alimshuhudia mchezaji wa bei ghali Costa akicheza dakika zote 90 huku Atletico Madrid ikishinda 1-0 dhidi ya Malaga Jumamosi.
Koke – mchezaji ambaye United wamekuwa wakihusishwa naye lakini hawana nia ya kumsajili mwezi huu – alifunga bao pekee kwenymchezo huo.
Cooke alikuwa mmoja wa watu wa benchi la Ufundi walioambatana na Moyes kutua Old Trafford wakitokea Everton na mpango huo ulimfanya asafiri kutoka pwani ya kusini ya Hispania hadi kaskazini mwa San Sebastian, kumuangalia mchezaji wa Atletico Bilbao, Herrara akicheza mechi ya kipigo cha 2-0 kwa Real Sociedad.
Costa, ambaye pia alitakiwa na Liverpool Agosti mwaka jana na hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kuhamia Chelsea na Arsenal, amekuwa mmoja wa washambuliaji gumzo Ulaya msimu huu, baada ya kufunga mabao 19 katika mechi 18 na kuisaidia timu yake kuwa mpinzani mkuu wa Barcelona katika mbio za ubingwa wa La Liga.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyekataa ofa ya uraia wa Hispania mwaka jana ili aichezee Brazil katika Kombe la Dunia, nchi yake halisi aliyozaliwa, alisaini Mkataba mpya na Atletico ili kumzuia kwenda Liverpool, lakini anaweza kuuzwa kwa Pauni Milioni 31.

DIEGO COSTA KUELEKEA STAMFORD BRIDGE MAPEMA JUNI


Klabu ya Chelsea imekubali kutoa kiasi cha pauni milioni 32 kwa Atletico Madrid kwaajili ya kukamilisha dili la kumsajili mshambuliji mahiri,Diego Costa.
Costa ambaye amekuwa muhimili mkubwa kwa klabu hiyo ya Uhispania ikiwa na uwezo wa kuchukua La Liga na Ligi ya mabingwa barani Ulaya mpaka sasa, amekuwa akihusishwa na kuhamia London huku Jose Mourinho akihitaji mshambuliaji hatari zaidi.
Mourinho alisisitiza mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza kuwa alikuwa na malengo ya kufanya usajili mkubwa sana Stamford Bridge katika kipindi cha soko la usajili haraka iwezekanavyo.
Dili la Costa halitarajiwi kutangazwa rasmi mpaka ifikapo mapema mwezi Juni mara baada ya michezo miwili mikubwa ambayo nyota huyo anapambana kuweza kuwa fiti kuisaidia timu yake.
Costa alipata majeraha ya misuli na alikosa mchezo waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya Malaga Jumapili,mchezo ambao iwapo Atletico wangeshinda wangekuwa
tayari wametwaa taji la La Liga msimu huu.
Atletico watasafiri mpaka Camp Nou kupambana na Barcelona siku ya Jumapili katika mchezo ambao utaamua kombe linaenda wapi na siku saba baadae watakutana na wapinzani wao wa Jiji,Real Madrid kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itakayopigwa Lisbon.
Chelsea walimaliza msimu wa 2013/14 katika nafasi ya tatu,pointi nne nyuma ya Manchester City na pointi mbili nyuma ya Liverpool huku rekodi yao ya kufunga magoli ikionekana ndiyo sababu ya kushindwa kwao kupata taji.
Kikosi cha darajani kilifunga magoli 71 ukilinganisha na magoli 102 ya Man City na 101 ya Liverpool na mchezaji mmoja pekee ndiye alikuwa
mhimili ambaye ni kiungo mshambuliaji Eden Hazard akifunga magoli 14.
Samuel Eto’o,Fernando Torres na Demba Ba walifunga jumla ya magoli 19 pekee wote kati yao hivyo kumshawishi Mourinho kutumia pesa nyingi kwaajili ya kupata saini ya mchezaji kama Costa ambaye amefunga magoli 27 kwenye michezo 33 ya La Liga msimu huu.