Friday, September 12, 2014

MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA MBEYA CITY VS VIPERS FC

Jumamosi hii kwenye uwanja wa Sokoine  kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Mbeya City Fc na Vipers FC (Zamani Bunamwaya Fc)ya Uganda . 

Mchezo huo unamepangwa kuanza saa       10:00. 

Vipers Fc inatarajiwa kuwasili Mbeya jioni ya leo ikitokea Entebbe kupitia  Dar Es Salaam ambapo Kiingilio kitakuwa Sh.3000
Hii ikiwa ni mabadiliko kutoka kiingilio  kilichotangazwa  awali cha sh.  5000

DISMAS  TEN
OFISA HABARI
MBEYA CITY COUNCIL FC.

Thursday, September 11, 2014

TAZAMA WASHINDI WA LIGI KUU TZ BARA TANGU MWAKA 1965-HADI LEO

Hawa ni washindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara tangu mwaka 1965. Katika rekodi hii klabu ya Yanga imetwaa taji hilo mara 24, Simba mara 18 na mtibwa mara 2, nyingine zote zilizopoa hapa zimetwaa mara moja. Tarehe 20 ligi itaanza tena ya msimu wa 2014/15, Je Unadhani timu gani ipo katika nafasi ya kushinda taji hilo msimu huu?
Washindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Tangu 1965 hadi leo
    1965 Sunderland (Sasa Simba SC)
    1966 Sunderland
    1967 Cosmopolitan
    1968 Yanga
    1969 Yanga
    1970 Yanga
    1971 Yanga
    1972 Yanga
    1973 Simba SC
    1974 Yanga
    1975 Mseto SC
    1976 Simba SC
    1977 Simba SC
    1978 Simba SC
    1979 Simba SC
    1980 Simba SC
    1981 Yanga
    1982 Pan Africans
    1983 Yanga
    1984 Simba SC
    1985 Yanga
    1986 Tukuyu Stars
    1987 Yanga
    1988 Coastal Union
    1989 Yanga
    1990 Simba SC
    1991 Yanga
    1992 Yanga
    1993 Yanga
    1994 Simba SC
    1995 Simba SC
    1996 Yanga
    1997 Yanga
    1998 Yanga
    1999 Mtibwa Sugar
    2000 Mtibwa Sugar
    2001 Simba SC
    2002 Yanga
    2003 Simba SC
    2004 Simba SC
    2005 Yanga
    2006 Yanga
    2007 Simba SC
    2007/08 Yanga
    2008/09 Yanga
    2009/2010 Simba SC
    2010/2011 Yanga
    2011/2012 Simba SC
    2012/2013 Yanga
    2013/2014 Azam FC
    2014/2015 ??.

WEKUNDU WA MSIMBAZI KUTIFUANA NA URA YA UGANDA

Simba Wekundu wa msimbazi SC kesho wanatarajia kushuka dimbani kuonyeshana kazi katika Mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki chini ya kocha Patrick Phiri dhidi ya timu ya mamlaka ya ukusanyaji wa mapato nchini Uganda, URA katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam katika mtanange utakao anza majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki.

Wakati huo huo jumamosi jioni, Simba itakuwa na mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mk
oani Mtwara katika maadhimisho ya ‘Ndanda fc Day’.

TAREHE NDONI YA TAIFA 2014 2014 YAPIGWA KALENDA

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limesogeza tarehe ya kufanyika kwa mashindano ya ngumi ya Taifa na sasa yatafanyika kuanzia tarehe 03-08/11/2014.Dar es salaam.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe 08-14/10/2014 Dar es salaam.
Sababu za kusogeza mashindano hayo ni kuyapisha mashindano ya ngumi ya kimataifa yaliyoandaliwa na chama cha ngumi wilaya ya Temeke yanayotarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, lakini pia ni kutoa nafasi zaidi kwa mikoa ili kujiandaa vizuri na kufanya mashindano ya kuwapata wawakilishi wa mikoa yao katika mashindano ya taifa.
BFT tunawataki maandalizi mema na tunatoa wito kwa maafisa michezo wa mikoa yote ya Tanzania bara kuhakikisha wanaleta wachezaji kutoka katika mikoa yao ili kuleta upinzani utakaopelekea kupata timu ya taifa iliyo bora kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara.
Aidha BFT inawapongeza kampuni ya simu za mkononi ya Z         antel kwa udhamini wa mashindano hayo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 10,000,000/=ambazo zitasaidia baadhi ya mahitaji ya msingi ya kufanikisha mashindano hayo.

MWAMBUSI ASEMA PHIRI, MAXIMO, ASEMA NGOMA DAKIKA 90.

KOCHA mkuu wa Mbeya City fc na kocha bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita, Juma Mwambusi, amewakaribisha makocha Patrick Phiri wa Simba na Marcio Maximo wa Yanga.
Akizungumza na mtandao huu, Mwambusi amesema kocha Phiri ana historia ya kufundisha soka la Tanzania kwa ngazi ya klabu wakati Maximo amefundisha timu ya Taifa, lakini wote wataleta changamoto nzuri kwake.

Wednesday, September 10, 2014

JE TUFIKA KUHUSU TAIFA STARS HII AMA NDIO MWISHO

Hakuna kitu kinawaumiza watanzania kuhusu kilio kikubwa cha wadau na wapenzi wa soka nchini Tanzania ni kuitaka serikali, TFF na vyama wanachama wake pamoja na klabu zote kuwekeza katika soka la vijana kwa manufaa ya Taifa.
Tatizo la soka la Tanzania ni la kimfumo. Hakujawa na njia sahihi ya kupata wachezaji na kusababisha kuborongo kwa muda mrefu.
Aina ya wachezaji wanaopatikana Tanzania ni wale wasiokuwa na misingi ya mpira tangu utotoni, kwasababu hakuna akademi za kisasa na hata za kawaida kwa maeneo mengi ya nchi hii, hivyo vijana wenye vipaji vya soka hujikuta hawana kwa kujiendeleza.
Soka la vijana ni muhimu na lazima Taifa kama Taifa liandae mpango mkakati wa kitaifa kwa malengo ya kuwa na falsafa ya Taifa na mfumo sahihi wa kuibua, kukuza na kulinda vipaji vya soka.
Marsh aliachishwa kazi ya kuinoa Stars sambamba na kocha Mdenish, Kim Poulsen kwa madai ya wawili hao kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa na Shirikisho la soka la Tanzania, TFF.
Hata hivyo wakati Kim anavunjiwa mkataba, Mashi alikuwa wodini akipata matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Usidhani huwa anakaa bure. Marsh ni moja ya watu wachache nchini wenye kiu ya kuona soka la nchi hii linapiga hatua.
Tangu mwaka 1991 anamiliki kituo chake cha kuibua, kulea na kukuza vipaji mkoani mwanza.

WADHAMINI WA VPL WAGAWA JEZI KWA TIMU ZA VPL KWA AJILI YA SEPT 20 VPL

Ikiwa zimebaki siku 10 kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2014-2015 wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom watoa jezi kwa vilabu vyote 14 vitakavyoshiriki ligi hiyo.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu za Ligi Kuu msimu mpya leo, Vodacom wamekabidhi jezi za rangi ya kijani na njano kwa Yanga na nyekundu na nyeupe kwa Simba, lakini muundo ni mmoja kila kitu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alihakikisha timu zote 14 za Ligi Kuu zinapatiwa vifaa hivyo.
Timu zote 14 zilituma wawakilishi wao katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam.  
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi, Azam FC wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo, wakati washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20.
Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumapili wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC.