Uongozi wa Mbeya
City umesema kuwa bado inatambua kuwa Deus Kaseke ni mwanandinga wao na kukanusha
uvumi wa kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kujiunga na Simba ama Yanga
kupitia dirisha dogo lililoanza kufunguliwa mnamo Nov 15/2014.
Kiungo huyo mshambuliaji wa
kikosi hicho cha Mbeya City, hivi karibuni jina lake limeoneka kuchukuwa nafasi katika vyombo vya habari ikionyesha kwamba mchezaji huyo anakwenda Msimbazi Simba sanjari na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Ame Ali ambapo mpaka sasa mtibwa imekanusha kupitia afisa habari wake Tobias kifaru akisema hawana mpango wakuuza mchezaji lakini kama kunatimu inataka mcheza ifike katika mashamba ya miwa.
Aidha taarifa hizo zimekuwa
zikidai kuwa mchezaji huyo huenda akamwaga wino katika klabu ya Yanga kwa ajili
ya kukipiga katika duru la pili .
Akiweka bayana kupitia Kapu la habari .blogspot.com Katibu mkuu wa klabu ya Mbeya ciity Emmanuel Kimb amesema mpaka sasa
uongozi huo haujapata ofa yoyote kutoka kwenye vilabu hivyo.
Amesema, hivyo
mchezaji Deus Kaseke anaendelea kuwa mchezaji halali wa klabu ya Mbeya City
lakini Kimbe, hakuwa tayari kuweka wazi mkataba walioingia na mchezaji huyo.
Katibu huyo ameweka wazi
kuwa Mpaka sasa bado klabu hiyo inauhalali wa kuendelea kumtumia mchezaji
Deus Kaseke kwani mkataba wake haujamalizika na pia uongozi haujapokea ofa
yoyote kutoka klabu za Yanga na Simba.
Sanjari na hayo Timu ya
mbeya city inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi huu kujiweka sawa michezo inayofuata ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara itakayo Endelea Dec 26/2014.
Timu hiyo ambayo itafungua
dimba na timu ya Ndanda kutoka Mkoani Mtwara, mchezo unaotaraji kupigwa kwenye
dimba la kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine Jijini Mbeya kwa sasa mbeya city ipo nafasi ya mwisho ya 14 ikiwa na point 5 katika Msimamo ya ligi hiyo kwa Mechi Saba zilizochezwa.
Tazama Matokeo ya Mbeya city:
Mechi
Dimba
1. Mbeya City 0-0 Jkt Ruvu Sokoine
2. Mbeya City1-0 Coastal Sokoine
3. R'Shooting 0-0 Mbeya Mabatini
4. Mbeya City0-1 Azam Sokoine
5. Mbeya City 0-2 Mtibwa Sokoine
6. Mgambo Jkt 2-1 Mbeya Mkwakwani
7. Stand United1-0 Mbeya Kambarage