Tuesday, December 16, 2014

YANGA WAKALI KWELI KWELI YAMTUPIA VIRAGO EMERSON NA KIIZA

Baada ya Mvutano wa hapa na pale nani aachwe kati ya Emerson kiiza na Coutinho Yanga sasa imeamua kuwaacha kuwatupia virago Mbrazil, Emerson de Oliviera Roque na Mganda Hamis Kiiza na kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mrundi Amisi Tambwe.
Tambwe amesaini Mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachwa na klabu yake, Simba SC aliyoichezea msimu mmoja uliopita akitokea Vital’O ya Burundi.
Yanga SC imeamua kumuacha Mbrazil Emerson baada ya kushindwa kupata Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Tambwe anaungana na Mliberia, Kpah Sherman, Wanyarwanda Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Mbrazil Andrey Coutinho kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni Yanga SC.
Wakati dirisha la usajili limefungwa jana Saa 6:00 usiku.
Yanga SC imesajili jumla ya wachezaji watatu wapya baada ya kumuacha Emerson, mwingine ni Danny Mrwanda. 
Katika kipindi cha msimu mmoja, Tambwe ameichezea Simba SC jumla ya mechi 43 na kuifungia mabao 26.
Maisha yake yalianza kuwa magumu Simba SC baada ya ujio wa kocha Mzambia, Patrick Phiri kuchukua mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic.

UONGOZI WA CLUB YANGA WASAMBARATISHA BENCHI LAKE LA UFUNDI

Uongozi wa club ya Yanga umewatupia virago Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Leiva na kuwarejesha Mholanzi, Hans van der Pluijm na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.
Maximo ametupiwa virago na baada ya kipindo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe.
Pluijm atamewasili  jana 8:38 usiku na kuweka kandarasi ya Mkataba wa kuanza kazi ambapo Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.
Maximo na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni.
Hata hivyo baada ya muda usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya kiufundi.
Pluijm alirudi Ghana wakati Mkwasa alirejea nyumbani Tanzania kabla ya kuajiriwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Mkufunzi Mkuu.
Hadi anaondoka Yanga SC, Maximo ameiongoza timu hiyo katika mechi 14, kati ya hizo akishinda 10, sare moja na kufungwa tatu dhidi ya Kagera Sugar 1-0, Mtibwa Sugar 2-0 sawa na Simba SC katika Mtani Jembe. 
Pluijm aliiongoza Yanga SC katika mechi 19, akishinda 11, sare sita na kufungwa mbili dhidi ya Al Ahly 1-0 Cairo na Mgambo JKT 2-1 Tanga.
Yanga SC ilikuwa tayari kuendelea na Maximo iwapo angekubali kufanya kazi na Mkwasa, lakini baada ya kukataa, klabu imeoana bora kuachana naye.
Maximo alikuwa anafanya kazi kwa mara ya pili Tanzania, baada ya awali kuwa kocha wa timu ya soka ya taia, Taifa Stars kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.
REKODI YA PLUIJM AIKIWA NA YANGA SC
Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa.
Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)

Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)

Sunday, December 14, 2014

VARANE AWEKA WAZI KUWA ILIKUWA KIDOGO ATUE MAN UNITED

BEKI wa Real Madrid, Raphael Varane amabainisha kuwa ilibaki kidogo ajiunge na Manchester United kabla ya kukamilisha usajili wake Santiago Bernabeu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, alijiunga na Madrid akitokea klabu ya Lens mwaka 2011 kwa kitita cha euro milioni 10.
Hata hivyo, Varane amekiri kuwa alikuwa akifikiria kwenda Old Trafford lakini akaamua kwenda Maddrid kwani aliona ndio mahali pazuri kwa kuimarika kama mchezaji.

Varane amesema walikuwa wamekaribia kukubaliana na United kwnai mama yake anazungumza lugha ya kiingereza hivyo ndio alikuwa kama mkalimani lakini baada ya kufikiri sana akaona bora aende Madrid.

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA HAPA NA PALE

Arsenal na Liverpool wanachuana Juventus katika kuwania saini ya beki wa kulia wa Barcelona Martin Montoya, mwenye 23 ambae amekosa namba kwenye kikosi cha barca.
Mshambuliaji Fernando Torres anaweza kurejea katika klabu yake ya Chelsea mwezi januari,Ac Milan wanampango wa kusitisha mkataba wake.
WENGER
Klabu yaNapol ya itali wanaangalia uwezekano wa kumsajili winga Yannick Bolasie, mwenye miaka 25 kutoka klabu ya Crystal Palace.
Brendan Rodgers
Timu ya Man United wako tayari kupamba na Real Madrid ili kuweza kupata saini ya kiungo Christoph Kramer anaekipiga na klabu ya Borussia Monchengladbach, pia kukiwa na tetesi beki.

ROGERS
Winga wa Chelsea Thorgan Hazard yuko tayari kujiunga na Borussia Monchengladbach kwa mkataba kamili baada ya kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza anakocheza kwa mkopo toka Chelsea.

Friday, December 12, 2014

BBC:HOFU YATANDA TANZANIA KUNYIMWA MSAADA NA MAREKANI

Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa na trilioni 1.1 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo.
Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.
Haya yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo.
Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.
Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.
Wanaotakiwa kuwajibishwa na Rais Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Novemba mwaka huu, Serikali ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo makubwa katika sekta ya nishati nchini.
Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.
Wakati wa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.
Juhudi za BBC kumtafuta Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress,aweze kuzungumzia juu ya ripoti hiyo ziligonga mwamba kutokana na sababu za kiprotokali .

EVERTON AJIPANGA KUMTIA KANDARASI MPYA SAMWEL ETOO

Wakala wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o anatarajiwa kuwa nchini Uingereza wakati wa krismasi ili kuzungumzia suala la kuongeza mkataba na klabu ya Everton.
Mkataba aliosaini mshambuliaji huyo wakati akitua Goodison Park kama mchezaji huru katika majira ya kiangazi una kipengele ambacho kinaruhusu mazungumzo kufanyika pindi mechi 15 zinazpokuwa zimechezwa.
Kutoka na umuhimu wa Eto,o katika klabu hiyo baada ya kufunga mabao manne na kusaidia mengine mawili katika mechi 15 za mashindano yote, Everton wanaonekana kuwa tayari na mazungumzo hayo.

 Mara kadhaa kocha wa Everton, Roberto Martinez amekiri kuwa angependa kumbakisha Eto’o mwenye umri wa miaka 33 katika kikosi chake.

WENGER AWA BABAISHA MASHABIKI KATIKA SUALA LA USAJILI

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amehatarisha kuwaudhi zaidi mashabiki wa timu hiyo baada ya kudai kuwa hatakuwa na haja ya kufanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwakani kama wachezaji wote katika kikosi chake cha sasa watakuwa fiti.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amekuwa katika shinikizo kubwa katika wiki za karibuni baada ya Arsenal kuonekana kushindwa mapema mbio za ubingwa kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City.
Wenger alishambuliwa na mashabiki wenye hasira katika kituo cha treni wakati akirejea London baada ya mchezo dhidi ya Stoke.
Pamoja na kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa alama 13 Wenger bado bado anaonesha kutoshtushwa na hali hiyo kwa kudai kuwa hatarajii usajili wa Januari kuwa pilikapilika kubwa.

Wenger amesema kama wachezaji watakuwa fiti na uwezo wa kucheza hadhani kama atahitaji kufanya usajili wa aina yeyote.