Majogoo wa jiji london Club ya soka ya Liverpool
imepiga chini ofa ya paundi milioni 30 waliyotoa Arsenal kwa ajili ya
kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez. Kumekuwa
na tetesi za muda mrefu za Suarez kutaka kuuzwa baada ya kufungiwa
mechi 10 kwa kumng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika Uwanja
wa Anfield msimu uliopita. Klabu
ya Real Madrid ya Hispania ndio wanaotegemewa kumsajili mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uruguay baada ya kutamka wazi kwamba ameyachoka
maisha ya Uingereza. Mwishoni
mwa wiki hii Arsenal nao walidaiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha
kumuwania lakini Liverpool walikataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na
tetesi hizo huku wakisisitiza kwamba bado wanamhitaji mshambuliaji huyo.Tuesday, July 9, 2013
LIVERPOOL YAIBWAGA CHINI OFA YA ARSENAL KUHUSU SUAREZ
Majogoo wa jiji london Club ya soka ya Liverpool
imepiga chini ofa ya paundi milioni 30 waliyotoa Arsenal kwa ajili ya
kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez. Kumekuwa
na tetesi za muda mrefu za Suarez kutaka kuuzwa baada ya kufungiwa
mechi 10 kwa kumng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika Uwanja
wa Anfield msimu uliopita. Klabu
ya Real Madrid ya Hispania ndio wanaotegemewa kumsajili mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uruguay baada ya kutamka wazi kwamba ameyachoka
maisha ya Uingereza. Mwishoni
mwa wiki hii Arsenal nao walidaiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha
kumuwania lakini Liverpool walikataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na
tetesi hizo huku wakisisitiza kwamba bado wanamhitaji mshambuliaji huyo.THIERRY HENRY NAYE YUMO KIKOSI CHA WACHEZAJI 10 WA MLS
Mshambuliaji nyota wa
zamani wa Ufaransa, Thierry Henry ni moja kati ya wanadinga nyota 10
watakaounda kikosi kutoka katika Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS
ambacho kitapambana na AS Roma ya Italia Julai 31 huko jijini Kansas. Henry
mwenye umri wa miaka 35 mshambuliaji wa klabu ya New York Red Bull
ambaye aliisadia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia mwaka 1998, amefunga
mabao sita katika mechi 17 alizoichezea timu hiyo msimu huu. Kabla ya kwenda Marekani mwaka 2010 akitokea klabu ya Barcelona, henry amewahi kucheza katika vilabu vya Juventus na Arsenal. Golikipa
wa FC Dallas ambaye ni raia wa Peru Raul Fernandez, kiungo wa timu ya
taifa ya Canada Will Johnson na Beki wa Kansas City Aurelien Collin
ambaye ni raia wa Ufaransa ni miongoni mwa wachezaji wasiokuwa raia wa
Marekani walioteuliwa katika kikosi hicho cha nyota wa MLS.
FIFA-SEPP BRATTER ATARAJI KUZUNGUMZA NA MAOFISA WA ISRAEL
![]() |
| Bratter akiyatafakari mazungumzo |
MESSI RASMI ATARAJIWA KUREJEA BARCA MAZOEZINI JULAI 15
Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa argentina na club ya fc Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kurejea mazoezini Julai 15
baada ya kupumzika kwa wiki moja pekee katika likizo yake kutokana na
majukumu mbalimbali ambayo yamekuwa yakimtinga. Masimu
wa 2012-2013 kwa mchezaji huyo nyota ulimalizika Juni 15 baada ya
Argentina kuigaragaza Guatemala kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kimataifa
wa kirafiki, hivyo kumanisha kwamba nyota huyo angekuwa na mwezi mzima
wa kupumzika kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Hata
hivyo Messi mwenye umri wa miaka 26 alitumia nafasi hiyo kucheza mechi
mbalimbali za hisani kuzunguka dunia na kumaliza ziara yake hiyo
mwishoni mwa wiki iliyopita huko Chicago, Marekani. Jumla
ya ziara zote hizo Messi amesafiri kilimita zaidi ya 90,000 toka msimu
wa ligi ulipomalizika akitembelea nchi za Argentina, Ecuador, Guatemala,
Italia, Senegal, Colombia, Peru na Marekani. Nyota
huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya msuli mwishoni mwa msimu
uliopita na mapumziko mafupi aatakayopata yatawapa uhakika mdogo
madaktari juu ya afya yake kabla ya kuanza msimu mpya wa 2013-2014. ROLNADO NAYE KUWANIA TUZO YA UNYAYO WA DHAHABU:
Mshambuliaji nyota mahiri wa club ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa katika orodha ya
wachezaji 10 watakaowania tuzo ya kiatu cha Dhahabu kwa mwaka 2013. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa ureno atakuwa mchezaji wa kwanza wan chi hiyo
kushinda tuzo hiyo ambayo ilianza kutolewa mwaka 2003 mahsusi kwa
wachezaji waliozidi umri wa miaka 28. Mchezaji
mwenzake wa Madri Iker Casillas na kiungo mahiri wa Barcelona Andres
Iniesta ni miongoni wa nyota wengine walioteuliwa kugombea tuzo hiyo. Wachezaji
waliwahi kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa kuangalia uwezo wake wa
kipindi chote alichocheza soka na kiwango chake cha sasa, ni pamoja na
Roberto Carlos, Ronaldinho, Francesco Totti na mshindi wa mwaka uliopita
Zlatan Ibrahimovic. Wachezaji
wanaweza kushinda tuzo hiyo mara moja pekee, ambapo sherehe zake
hufanyika jijini Monaco kila mwaka toka ilipoanzishwa. Mbali
na hao wengine waliokuwemo katika orodha ya mwaka huu ni pamoja na
Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala, Andrea Pirlo anayekipiga
Juventus, Didier Drogba kutoka Galatasaray, Frank Lampard-Chelsea,
Miroslav Klose-Lazio, David Trezeguet-River Plate and David
Beckham-Paris Saint-Germain.
Sunday, July 7, 2013
STEWART HALL AMKUBALI KASEJA ASEMA BADO NI BONGE LA KIPA TZ"
![]() |
| Stewart hall akitabasamu kwa pozi la aina yake |
Hall amesema kipa wake mwingine "Jackson Wandwi anafikiria kumpeleka kucheza kwa mkopo katika Club ya Ashanti United ya Ilala iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ili kupata uzoefu baadaye arejee kushindana na Mwadini na Aishi.
“Aidha Hall amesema nafahamu fika kuwa Kaseja ametupiwa virago MSimbazi na nasikia watu wanamzungumzia sana wakimhusisha na Azam fc. Mimi nakubali yule ni kipa mzuri na ana uzoefu. Ila mimi nina makipa wazuri wawili, Aishi na Mwadini. Nataka hawa washindane ili kumpata kipa nambari moja wa timu"
Hata hivyo Hall amesema kuwa bado Azam ina makipa wengine wazuri wa timu za vijana, ambao watakuwa wakipewa nafasi ya kujifua na kikosi cha kwanza msimu ujao.
“Hivyo nitakuwa na Aishi na Mwadini kama makipa wawili imara wa timu ya kwanza, maana yake Wandwi ataendelea kupoteza kiwango chake. hivyo nifikiria bora nimpeleke Ashanti ili akakuze kipaji chake na kupata uzoefu, baadaye arejee kwenye timu akiwa imara zaidi".
Mbali na hilo tulipomuuliza kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara na michuano ya kombe la shirikisho barani afrika Hall amesema kwamba Azam
ambayo itaipeperusha bendera ya Tanzania kwa mara ya pili mfululizo kwenye Kombe la
Shirikisho Afrika mwakani, iko katika mazoezi.
“Tunaendelea na mazoezi ya msimu mpya. Kwa sasa tupo katika programu ya ufukweni na gym. Baada ya hapo tutaanza programu rasmi ya uwanjani. Lakini wiki mbili za mwanzo za Agosti tutakwenda Afrika Kusini kuweka kambi,”.
“Tunaendelea na mazoezi ya msimu mpya. Kwa sasa tupo katika programu ya ufukweni na gym. Baada ya hapo tutaanza programu rasmi ya uwanjani. Lakini wiki mbili za mwanzo za Agosti tutakwenda Afrika Kusini kuweka kambi,”.
MARION AFANIKIWA KUTWAA TAJI LA KWANZA LA MICHUANO YA GRAND SLAM.
Marion Bartoli mwanadada nyota katika
tenisi, amefanikiwa kushinda taji lake la kwanza la
michuano ya Grand Slam baada ya kumchalaza Sabine Lisicki wa Ujerumani
kwa seti 6-1 6-4 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon. Bartoli
ambaye anashika namba 15 katika orodha za ubora kwa upande wanawake
alitumia dakika 30 pekee kushinda seti ya kwanza wakati mpinzani wake
Lisicki akionekana kushindwa kumudu vishindo katika fainali yake ya
kwanza ya Grand Slam. Akihojiwa
mara baada ya mchezo huo Bartoli amesema haamini kama amenyakuwa taji
hilo na alikuwa akijisikia kucheza kwa kiwango chake cha juu huku kila
kitu alichofanya kikimuendea sawa. Michuano
hiyo inaendelea tena baadae kwa mchezo wa fainali kwa upande wa wanaume
ambapo Andy Murray wa Uingereza anayeshika namba mbili katika orodha za
ubora atachuana na Novak Djokovic wa Serbia anayeshika namba moja
katika orodha za ubora.
Subscribe to:
Posts (Atom)





