Martina Hingis ambae ni mwanadada nyota wa
tenisi wa zamani, kutoka Switzerland anatarajiwa kurejea
tena katika ulingo wa tenisi baada ya kustaafu mchezo huo mwaka 2007. Hingis
mwenye umri wa miaka 32 amekubali mwaliko wa kucheza michuano ya wazi
ya California ya wawili wawili akiwa sambamba na Daniela Hantuchova
baadae mwezi huu. Nyota
huyo ambaye amewahi kushinda mataji matano ya Grand Slam kwa mchezaji
mmoja mmoja likiwemo taji la Wimbledon mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka
16, Jumamosi iliyopita alichaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji mashuhuri
wa mchezo huo kuwahi kutokea. Akihojiwa
kuhusiana na uamuzi huo wa kurejea uwanjani baada ya kupita kipindi
kirefu, Hingis ambaye pia amewahi kushika namba moja katika orodha za
ubora duniani kwa upande wa wanawake amesema bado anahisi kuwa na ari ya
ushindani ndani ya nafsi yake. Mara
ya kwanza Hingis alistaafu mchezo huo akiwa na miaka 22 baada ya
kusumbuliwa na majeraha lakini alirejea tena mwaka 2006 kabla ya
kustaafu tena mwaka 2007 baada ya kukutwa na chembechembe ya dawa za
kusisimua misuli ingawa mwenyewe alikana tuhuma hizo.
Wednesday, July 17, 2013
CAF YATANGAZA KUSOGEZA MBELE MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA KATI YA WATANI WA JADI"
Shirikisho la kandanda Barani Afrika-CAF limesogeza mbele mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika
ambao unawakutanisha watani wa jadi nchini Misri timu za Zamalek na Al Ahly
mpaka Jumatatu ijayo.
Vigogo
hao wa soka nchini humo walitarajiwa kucheza Jumapili katika mji wa El
Gouna ambao uko kilometa 500 kutoka mji mkuu wa Cairo kutokana na sababu
za kiusalama. Katika
taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Zamalek, wamethibitisha kuwa FIFA
imekubali mchezo huo kuchezwa El Gouna pamoja na kwamba uwanja huo
haukuwepo katika ratiba za michuano hiyo na kuamua kuchelewesha mchezo
huo kwa siku moja kwasababu za kibiashara. Wizara
ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ilikataa mapema kuhakikisha usalama wa
mechi hiyo kuchezwa jijini Cairo au Alexandria kabla ya Zamalek kuchagua
El Gouna.

WAKALA WA SUAREZ ASEMA KAMA KUNA CLUB INAMTAKA MCHEZAJI HUYO IWEKE MEZANI KITITA CHA NGUVU
Wakala
wa mshambulaij nyota wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uruguay" Luis Suarez’ amebainisha na kuweka wazi kama kuna klabu
inahitaji kumsajili nyota huyo lazima iandae dau la nono la pauni miliaoni
40 ili kupata huduma yake.
Klabu
ya Liverpool imesema itasikiliza ofa ya pauni milioni 40, lakini kuna
uwezekano wa ofa hiyo kupanda mpaka kufikia pauni milioni 50 kumnunua
nyota huyo mwenye matukio ya aina yake nchini England, likiwemo la
kumng`ata beki wa Chelsea, Ivanovic na kusimamishwa mechi kumi, pamoja
na tuhuma za ubaguzi wa rangi kwa beki wa mabingwa wa soka nchini
Englanda, Manchester United, Mfaransa Patrick Evra.
Wakala
wa Suarez bwana Pere Guardiola, ambaye ni kaka yake kocha wa wekundu wa
kusini mwa Ujerumani, The Bavarian, klabu ya Bayern Munich , Joseph
Pep Guardiola , amasema atakaa mezani na klabu yoyote yenye uwezo wa
kuweka mezani mzigo wa pauni milioni 40.
Ambapo sasa Baadhi ya Klabu kubwa barani Ulaya zinataka kuinasa saini ya Luis Suarez kutoka kwa majogoo wa jiji.
Arsenal
ni klabu pekee yenye mpango wa nguvu zaidi kutaka kumsajili Suarez kwa
pauni milioni 35, lakini ofa hiyo inaonkana haina maana kwa wekundu wa
Anfield waliotangaza pauni milioni 40.

Saurez
ambaye atajiunga na Liverpool waliopo Melbourne jumatatu ijayo, ana
mkataba na Liverpool mpaka mwaka 2016. Lakini Liver wameonekana kuwa na
msimamo wa kumbakisha, huku klabu za Arsena, Real Madrid na Chelsea
zakiimarisha rada zao kutaka kumsajili.
UONGOZI WA YANGA WAWATAKA MASHABIKI KUJITOKEZA KWA WINGI"
Club ya Yanga ya jangwani kupitia uongozi wake
waumewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi
ya kimataifa ya kirafiki itakayochezwa Julai 18 mwaka huu.
Mechi hiyo kimataifa ya Kirafiki dhidi ya timu ya
3 Pillars ya Nigeria inataraji kutimua vumbi Julai 18 mwaka huu katika uwanja wa
Taifa.
Mechi
hiyo ni sehemu ya maandalizi ya klabu zote mbili kabla ya ligi kuu
kuanza mwezi ujao ambapo Yanga pia inajinoa kwa ajili ya michuano ya
ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mratibu
wa mechi Salum Mkemi amesema kikosi cha wachezaji 17 na viongozi na
makocha wao wapo jijini Dar es Salaam wakijifua kwa ajili mtanange huo
utakaochezwa katika uwanja wa Taifa.
Mkemi
amesema pia timu ya 3 Pillars ambayo imepanda daraja la ligi kuu nchini
Nigeria inataraji kujipima na Coastal Union ya Tanga huku wakifanya
mazungumzo na Mbeya City kwa ajili ya mechi nyingine za Kirafiki.
Katibu
mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amesema wachezaji wako kambini
kujiwinda na michuano ya ligi kuu na kuongeza kuwa wana morali kuelekea
mchezo huo.
Mratibu
wa mechi ametangaza Viingilio vya mechi hiyo vitakuwa kati ya shilingi
elfu tatu na elfu 15 ili kuwawezesha mashabiki wengi zaidi kuhudhuria
kipute hicho.
Timu ya 3 Pillars inataraji kurejea nchini Nigeria Julai 30 mwaka huu.
Tuesday, July 16, 2013
KUTOA OFA PAUNI MILIONI 40 KUMNUNUA HULK--CHELSEA
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ana
nia ya kuongeza safu yake ya Ushambuliaji na tayari ameshamnunua
Mchezaji wa Germany Andre Schurrle huku kukiwa na tetesi Mastraika wa
sasa, Fernando Torres na Demba Ba, huenda wakapigwa bei.
Katika Msimu wake wa kwanza na Zenit,
Hulk alifunga Bao 11 katika Mechi 30 na kabla hajahamia huko Urusi,
akiwa huko Portugal na FC Porto, Hulk aliifungia Klabu hiyo Bao 54
katika Mechi 99 za Primera Liga na Jumla ya Mabao yake kwa FC Porto ni
78.
Inadaiwa Chelsea imetoa Ofa ya kwanza ya Pauni Milioni 40 kwa Mchezaji alienunuliwa Septemba Mwaka Jana kwa Pauni Milioni 35.
SIMBA YAJA NA MKUTANO MKUU JALAI 20 MWAKA HUU VS TBL"
Club ya soka ya Simba, inatarajia kufanya wake Mkutano Mkuu Jumamosi Julai 20 na Mdhamini wao,
TBL, Tanzania Breweries Limited ambapo mdhamini huyo ametoa Shilingi Milioni 20 ili kuendesha Mkutano huo.
Mkutanno Mkuu huo ni fursa safi kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, kuwasilisha Ripoti ya shughuli za Klabu hiyo.
TBL, ambayo ina Mikataba ya Miaka mitano
mitano ya kuzidhamini Yanga na Simba kuanzia Miaka miwili iliyopita,
inawajibika kuzipa Klabu hizo Shilingi Milioni 20 kila mmoja ili
kuendesha Mikutano Mikuu ya Vilabu vyao.
Akiongea wakati akikabidhi Cheki ya
Shilingi Milioni 20 kwa Simba, George Kavishe, Meneja wa Bia ya aina ya
Kilimanjaro Premium Lager, alisema: "Kama Wadhamini wakuu, tunatoa Fedha
hizi kama jukumu letu kwa Klabu ili iwajibike, ipate mafanikio nje na
ndani ya Uwanja. Tunaamini Mkutano huu utaimarisha uhusiano kati ya
Simba na Wanachama wake kwa kuwapa nafasi kupitia masuala ya Klabu yao
waipendayo."
Nae Katibu Mkuu wa Simba, Evodius
Mtawala, aliishukuru TBL kwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Mkataba
na akaahidi Fedha hizo zitatumika kama ilivyokusudiwa.
Kwa baadhi ya Wadau wa Simba Mkutano
Mkuu huu unasubiriwa kwa hamu kubwa hasa baada ya Klabu hiyo kugubikwa
na mfarakano na Mwezi Machi Kikundi kimoja cha waliodaiwa kuwa Wanachama
kujaribu kumpindua Rage kwa madai ya kushindwa kuongoza lakini jaribio
hilo halikufua dafu.
Pia, inasemekana ipo Kambi ya Wanachama
itakayoshika bango waelezwe kinagaubaga nini kimetokea kuhusu kuuzwa kwa
Straika wao kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, kwa Klabu ya Tunisia Etoile
Sportive Du Sahel Mwezi Januari kwa Dau linalodaiwa kuwa Dola Laki 3 na
Klabu kutolipwa Fedha hizo hadi sasa.
Wengine watapenda wajue nini kiliwasibu
Msimu uliopita na kumalizika Mwezi Mei huku Simba ikinyang’anywa Taji
lao la Ubingwa na Mahasimu wao wakubwa, Yanga, na pia kujikuta
wakibwagwa hadi Nafasi ya 3 nyuma ya Yanga na Azam na hivyo kutopata
fursa ya kucheza Mashindano ya Klabu Barani Afrika Mwakani.
FABREGAS ASEMA AMWAMBIA VILANOVA NATAKA KUBAKI HAPA"
Meneja wa Manchester United, David Moyes huenda akapata pigo lingine baada ya
kiungo wa FC Barcelona, Cesc Fabregas kumweleza kocha wake Tito
Vilanova kuwa anataka kubakia ndani ya club ya Barcelona wazee wa Katalunya.
Ambapo Jana julai 15 Man united walithibitisha kutuma ofa ya pauni milioni 26 ili kumsajili
Febregas, nahodha wa zamani wa washika bunduki wa kaskazini mwa London,
klabu ya Asernal.
Dili
la kumhitaji Febregas limekuja baada ya Thiago Alcantara kujiunga na
kocha wake wa zamani Pep Guardiola
katika klabu ya Bayern Munich badala
ya kujiunga ma mabingwa wa ligi kuu soka nchini England, Manchester
United.
![]() |
Wachezaji wa Barcelona wakiwa mazoezini kwa ajili ya msimu mpya wa La Liga |
Mambo
yamekuwa magumu kwa United baada ya kocha wa Barca Tito Vilanova kuweka
wazi kuwa amezungumza na Febregas ambaye amesema anataka kubakia Camp
Nou.
Vilanova
alisema: ‘Cesc amepokea ofa kutoka klabu nyingine. Nilizungumza naye na
ameniambia anataka kubakia hapa. Ndoto yake ni kutwaa makombe hapa”
“Tunafurahi
kuwa na Cesc. Nafahamu amepata ofa nyingi, lakini ameniambia kuwa, ana
furaja ya kuwepo Barca, hakuna haja ya kuondoka.’
Subscribe to:
Posts (Atom)