Monday, August 25, 2014

KUFUATIA KIFO CHA MCHEZAJI ALGERIA YASIMAMISHA LIGI

SHIRIKISHO la Soka nchini Algeria limesimamisha Ligi Kuu kufuatia kifo cha mchezaji wa Cameroon Albert Ebosse ambaye alipigwa na jiwe lililorushwa na mashabiki. Uamuzi huo umefikiwa jana katika kikao kilichofanyika jana. Ebosse mwenye umri wa miaka 24 alipigwa na jiwe kichwani wakati akitoka uwanjani baada ya timu yake ya JS Kabylie kufungwa na USM Alger huko Tizi Ouzou juzi. Tayari mamlaka inayohusika imeshaufungia Uwanja wa 1st Novemba 1954 kulikotokea tukio hilo. Shirikisho hilo pia limeamua kutoa ubani wa dola 100,000 kwa familia ya Ebosse kiwango ambacho kinaaminika angeweza kukipata katika kipindi cha mkataba wake huku wachezaji wa Kabylie nao wakitoa mishahara yao ya mwezi kama rambirambi ya kufariki kwa mwenzao. Imegundulika kuwa uwanja wa 1st Novemba 1954 ulikuwa katika matengenezo wakati wa mchezo huo na mashabiki walitumiwe mawe ya ujenzi yaliyokuwa yamewekwa maeneo hayo.

Albert Ebossé Bodjongo
Taarifa binafsi
Full nameAlbert Dominique Ebossé Bodjongo Dika
Date of birth6 October 1989
Place of birthDoualaCameroon
Date of death23 August 2014 (aged 24)
Place of deathTizi OuzouAlgeria
Height1.85 m (6 ft 1 in)
Playing positionForward
Timu ya ukubwani
YearsTeamMechiGoli
2008–2010Coton Sport FC
2010–2011Unisport Bafang
2011–2012Douala AC10(9)
2012–2013Perak FA16(11)
2013–2014JS Kabylie32(19)
Timu ya taifa
2009Cameroon U20

RONALDO YUKO POA SANA KUIKABILI CORDOBA.

MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kuanza katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Cordoba pamoja na kushambuliwa na majeruhi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alitokea benchi katika mchezo wa Super Cup uliochezwa Ijumaa iliyopita na kufungwa na Atletico Madrid. Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti amesema Ronaldo amefanya mazoezi vyema hivyo anaweza kumpanga katika kikosi chake. Ancelottio alikiri kuwa wakati wa maandalizi ya msimu alikuwa akisumbuliwa na majeruhi hivyo anahitaji kufanya jitihada ili aweze kurejea katika kiwangop chake. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 ambaye anashikilia tuzo ya mchezaji bora wa dunia alipata majeruhi ya mgongo wakati timu hizo mbili zilipotoa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza.
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo - Croatia vs. Portugal, 10th June 2013.jpg
Ronaldo playing for Portugal in 2013
Taarifa Binafsi
Full nameCristiano Ronaldo dos Santos Aveiro
Date of birth5 February 1985 (age 29)[1]
Place of birthFunchalMadeira, Portugal
Height1.85 m (6 ft 1 in)[2]
Playing positionForward
Club anayocheza
Current team
Real Madrid
Number7
acadaemy
1992–1995Andorinha
1995–1997Nacional
1997–2002Sporting CP
Timu za ukubwani
YearsTeamMechiGoli
2002–2003Sporting CP25(3)
2003–2009Manchester United196(84)
2009–Real Madrid165(177)
Timu ya taifa
2001Portugal U159(7)
2001–2002Portugal U177(5)
2003Portugal U205(1)
2002–2003Portugal U2110(3)
2004Portugal U233(2)
2003–Portugal114(50)

TFF YAOMBA KUANDA MECHI ZA MASHINDANO YA AFCON 2017

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais wake, Jamal Malinzi, limeomba kuadaa mashindano ya Kombe la Taifa Africa (Afcon).
TFF imetuma barua kwa Shirkisho la Soka Afrika (Caf) kuomba kuandaa mashindano yatakayofanyika 2017.

TFF imechukau uamuzi huo baada ya Caf kuifuta Libya iliyopanga kuandaa michuano hiyo mwaka 2017 kutokana na vurugu.

TFF imesema inaamini kuna miundombinu ya kutosha kuandaa michuano hiyo na tayari barua imetumwa Caf.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine amesema barua ya maombi kwenda imeshatumwa. 

WAMBURA HUYOO SASA MKURUGENZI WA MASHINDANO TFF

Aliyekuwa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Nyota emeendelea kunga’aa katika anga la kichezo ambapo sasa atakuwa Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo.

Wambura amepata nafasi hiyo baada ya TFF kuamua kumpandisha cheo na sasa anaicha ile nafasi yake ya ofisa habari.


Katibu Mkuu wa TFF, Mwesugwa Celestine ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar.

STARS KUKIPIGA NA MOROCCO DECEMBER 5 MWAKA HUU KIRAFIKI

Timu ya Tanzania Taifa Stars inataraji kwenda Morocco kukipiga na wenyeji wake katika mechi ya kirafiki ndani ya tarehe za Fifa.
Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Septemba 5 nchini Morocco.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine amesema wamepokea mwaliko na tayari Kocha Mart Nooij ameishatangaza kikosi chake.
Mwesingwa amesema Septemba 5 ni tarehe ambayo iko ndani ya tarehe za Fifa, hivyo maandalizi yanaanza na kocha ameishaita kikosi.

Stars katika mechi yake ya mwisho, Stars ilichapwa kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini nchini Msumbuji na kutolewa katika mbio za kuwania kucheza michuano ya Mataifa Afrika.

Thursday, August 21, 2014

YANGA YAITUNGUA 1-0 CHIPUKIZI YA ZANZIBAR KATIKA MECHI YA KIRAFIKI

DSC_0018Club ya yanga imefanikiwa kuitandika bao 1-0 dhidi ya Chipukizi FC ya Zanzibar katika mchezo wa kwanza wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Mbrazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ katika dakika ya 6 ya mchezo.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa kocha wa Yanga,  Mbrazil, Marcio Maximo kuwaona wachezaji wake wakicheza mechi ya kirafiki.
Ili kuhakikisha anawaona wachezaji wote, Maximo alitumia vikosi viwili tofauti kwa kila kipindi.

Wednesday, August 20, 2014

AZAM NJE KOMBE LA KAGAME KWA PENALT 4-3.

MABINGWA wa Tanzania VPL, Azam fc wametolewa nje katika michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame kwa kufungwa penalty 4-3 dhidi ya El Merreik ya Sudan  katika mchezo wa robo fainali.
Mshindi wa mchezo huo uliopigwa katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda, alilazimika kupatikana kwa changamoto ya matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana (0-0)