
Arsene Wenger anataka kipa mzoefu atengeneze ushindani kwa Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Mazungumzo
baina ya wawakilishi wa Cesar na viongozi wa Gunners tayari
yamefanyika, lakini hayajamalizika kwa kuwa kipa huyo yupo kwenye
majukumu ya kimataifa.

ARSENAL sasa inatarajiwa kumaliza dili hilo mara moja tu, baada ya
kubainika Roma ya Italia nayo imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya
Cesar.
Kipa
huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yupo huru kuondoka Loftus Road
kufuatia kushuka kwa QPR hadi Championship, anataka kubaki London ambako
amezoea maisha tangu awasili msimu uliopita akitokea Inter Milan.
Na
The Gunners – ambayo inatumai kukamilisha pia usajili wa Gonzalo
Higuain wiki ijayo, baada ya kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti
kufungua njia kwa mshambuliaji huyo kuondoka Hispania – inajiamini dili
hilo litakamilishwa baada ya Fainali ya Kombe la Mabara Jumapili.
Wenger
alitaka kusajili kipa wa Stoke, Asmir Begovic na wa Liverpool, Pepe
Reina lakini, licha ya kuwa na fungu la bajeti ya usajili la Pauni
Milioni 70, kocha huyo wa Arsenal ameona hana sababu ya kutumia fedha
nyingi kwa ajili ya kipa.
Rangers
itasikiliza ofa ya kiasi cha Pauni Milioni 2 kwa Cesar, wakati mshahara
wake wa Pauni 70,000 kwa wiki halitakuwa tatizo kwa The Gunners, ambayo
imetuma waangalia vipaji wake nchini Brazil kumuangalia Cesar
anachokifanya katika Kombe la Mabara.
Pamoja
na mpango wa kuwasajili Cesar na Higuain, The Gunners pia wanataka
kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams na kiungo wa Everton,
Marouane Fellaini. Lakini masuala ya kifedha yanatia saka kama Arsenal itaweza kusajili wachezaji wote hao.
Hadi
sasa, Arsenal imegoma kumpa Fellaini mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki
na pia imeshindwa kufika dau la Pauni Milioni 24 za kumnunua.
